Mtangazaji na meneja wa vipindi wa kituo cha runinga cha DTV, Penniel Mwingila aka VJ Penny, amesema kuwa yeye na mpenzi wake, staa wa ‘My Number One’, Diamond Platnumz, wamepeana nafasi ili kila mmoja kutafakari anachotaka maishani.
Kauli ya Penny kwenye mahojiano maalum na Bongo5 TV, inajibu maswali ya wengi kuhusiana na kama wawili hao wapo pamoja au wameachana baada ya Diamond na mpenzi wake wa zamani, Wema Sepetu kurudiana tena. Katika interview hiyo, Penny ameongea pia kuanzia historia yake, namna alivyoingia kwenye utangazaji, alivyokutana na Diamond, mapenzi yao yalivyokuwa, alivyojisikia baada ya kuona picha za Wema na Diamond, maisha yake ya sasa na mipango yake ya mwaka huu.
Akizungumzia kuhusu alivyojisikia baada ya kuona picha za Diamond akiwa na Wema, Penny amesema yeye pia alishangaa kama watu wengine walivyoshangaa kuziona.
“Mimi ni mtu ambaye utaniambia ‘fulani amefariki’ na sitakiamini mpaka nione kabisa huyu hapa amekufa,” amesema Penny. “Nilipoziona picha nilishtuka kidogo, kibinadamu nilikuwa ‘Ohh Mungu wangu kipi kinaendelea’. Lakini sijui.. Mungu wa ajabu sana, niliichukulia kwa uzito mdogo kadri nilivyoweza, ilipita tu kama ‘shaaa’.. na dakika inayofuata (Diamond) anasema ‘ohh ni movie’. Mimi nilikuwa kama nyie, amini usiamini ‘Ni movie okay vizuri, baby anafanya movie’. Kwa kawaida nilitakuwa kuipokea tofauti lakini ni kama nilishikwa na ganzi kwa muda, sikutaka kujiumiza. Kuna ‘buttom’ ambayo nikiruhusu iniumize nitaumia, nikiamua kitu kinipite na siwezi hata kujisumbua. Alirejea, maisha yakaendelea, nimekaa nasubiri movie hiyo.”
Penny amesema pamoja na yote hayo, maisha yaliendelea kama kawaida kati yao kama vile hakuna kilichotokea.
“Alirejea kutoka kwenye safari yake ya movie na tuliendelea kuwa pamoja kwasababu mimi nilikuwa nani kuhukumu tofauti? Hicho ndicho kitu nawaambia watu, sikuwepo hivyo kama anasema alikuwa anafanya movie nitamuamini kwasababu sikuwepo. Napenda kuona vitu mwenyewe, mimi ni mtu wa hivyo, nahukumu vitu pindi nionapo mwenyewe. Maisha yaliendelea, tuliendelea kuwa sisi. Nilikuwa na vitu vilivyokuwa vikizunguka kwenye mawazo yangu nje na ndani.. ‘hivi ndivyo natakiwa kuwa?’ Watu wanadhani nina moyo wa jiwe, nina moyo, nina akili, saa zingine inabidi nikae nifikirie, nini hiki, nini kile. Mambo yalikuwa sawa lakini tofauti kidogo kuzingatia ukweli kwamba sikujua nini cha kufikiria, sikujua nini cha kufanya na nilitakiwa kuchukua muda wangu kuhakikisha kuwa sifanyi kosa lolote. Na nilikuwa bado pembeni yake, bado nikimsupport chochote alichokuwa akikifanya iwe movie, nyimbo zake mpya au chochote, niliendelea kuwepo kwaajili yake kuwa girlfriend wake, rafiki yake wa dhati, mkono wake wa kulia.”
Hata hivyo Penny amesema ilifika wakati ambapo waliona bora ‘kupumzisha’ uhusiano wao kutokana na hali halisi ya mabadiliko yaliyokuwa yamejitokeza.
“Kama uhusiano wowote ulivyo, kuna mwanzo na mwisho na watu wanaachana kwa sababu nyingi. Nilihisi kwamba nahitaji kumpa nafasi, wote ni vijana na wakati mwingine tunahitaji nafasi kugundua vitu vipya, kuona kipi hasa unachokihitaji kwenye maisha. Unajua ukimruhusu ndege afanye vitu mbalimbali then atajua kama ‘mti huu ndio unanifaa, mti huu haunifai. Hivyo nilihisi kwamba wote tulihitaji hicho, tulihitaji ‘space’ hivyo nikampa nafasi na mimi nakuchukua nafasi. Huwa nawaambia watu kuwa vyovyote ilivyo, yeyote atakayekuwa naye, nipo pembeni yake nikimshangilia kwasababu ni kweli (Diamond) ni mtu mzuri ndani. Achana na watu wanavyomuona chizi chizi, sahau msanii unayemjua, ana roho nzuri na anajua anachokitaka. Ni ngumu kuacha iende.. kama ni rahisi kuacha iende basi hujampenda huyo mtu.”
Amesema kila anapoulizwa maswali ya ni nani kati yake na Diamond aliyemwacha mwenzake, hujibu hajui kwakuwa wamepeana tu nafasi ya kila mtu kufanya mambo yake na kuongeza kuwa bado wanaendelea kuwasiliana huku akiwa na furaha na chochote (Diamond) anachofanya.
Penny amesema japo ameendelea na maisha yake lakini bado anachukua muda kufikiria nini anachohitaji maishani na hadi sasa hajafikiria kuwa na mwanaume mwingine. “Bado, sio kwamba sitongozwi, wanaume wanakuja lakini najaribu … hakuna mwanaume mkamilifu, najaribu kutafuta mwanaume anayeweza kuwa mkamilifu kidogo najua yupo sehemu.”
Ameongeza kuwa anatamani kurejea katika maisha ya kawaida na kuwa na uhusiano na mwanaume asiye maarufu kwakuwa kuwa na uhusiano na mtu mwenye jina kulimfanya achunguzwe muda wote na kujikuta akikosa maisha ‘faragha’.
“Napenda kurejea kwenye maisha niliyokuwa nayo ‘it was much fun’, napenda maisha yangu ya faragha.”
Penny amesisitiza kuwa mwaka 2014 ameupanga kuwa mwaka wa kufanya kazi zaidi na anaamini utakuwa wa ushindi kwake.
“Nilijiambia mwenyewe siku ya January 1 kuwa ‘mwaka huu ni mwaka wa ushindi kwangu’ na naenda kushinda, vyovyote vile naenda kushinda, naenda kuweka nguvu yangu yote, kwahiyo kuna mengi yanakuja, mengi.”
Source:Bongo5.com
PENNY AAMUA KUFUNGUKA KUHUSU KUVUNJIKA MAPENZI YAO NA DIAMOND..HUU NDIO UKWELI NA NINI KINAENDELEA SASA
25
January 24, 2014
Tags
hana lolote anatafuta umaarufu tu huyo kabayaa ashukuru kutombwa na diamond kajulikana maana hata hicho kipindi chake sijui nani hua anaangalia
ReplyDeleteWaraka ulivyoandikwa kwa adabu jibu tushapata penny ajamuacha platinum ,platinum ndio kamuacha demu,mi nilitaka kushangaa penny amuache Domo ?noway,mademu Wa kibongo wanapenda maisha ya miteremko tafuteni vyenuuuuu mamae zenu.
DeleteIwe funzo, penny alikosea sana kuruhusu diamond kumrekodi wema tena na yeye akajifanya kumsema wema ulivuka mipaka dada ulitakiwa ku deal na diamond, diamond ndio a deal na wema wenzio wanagombana badae wanasuruhisha wakiwa kitandani ww haupo...
ReplyDeleteWema akiachwa penny anarudi,mark my word.zamani kushare mboo ilikuwa kosa la jinai siku hizi wadada Wa mujini kwa raha zenuuuu
Deletebabu yako baba yako na hata we mwenyewe hujulikani inamaana hwezi fanya maisha yako yakasonga we mdau hapo juu....mwacheni dads wa watu aishi maisha yake her life her choices kwaza n mdg et kabaya we mzur wote tumeumbwa na huyo huyo alokupa ww uzur..km unaliwa vile ovyooo. ndio povu limentoka na ndio nalipwa dada wa watu kutombwa na domo imekuwa km n nuksi khaaa oooh Madam mzr uzur autoe wapi kwi kwiiii
ReplyDeletePenny fanya kazi yako , achana na Diamond coz amekipata alicho kuwa anakihitaji toka kwako..now hana mpango na wewe! Girl move on please, wewe ni mzuri na Mungu atakujalia mwanaume mwingine atakae kufaa na kukuheshimu. Acha kujishusha ooh namsaport oh nakuheshimu, Diamond hana heshima na wewe my dear! Move on ooh
ReplyDeletePenny anabembeleza penzi lirudi nyie mnasemajeeeee?
DeleteKumbe na ww umeona
DeletePenny kaongea vzr sana, sikujua ana akili ya aina hii. mtu anaemtukana lazima ni taahira tu, wasichana wote mjini wanatombwa ovyo tu mbona, why mnamuona penny kama mkosaji hivo? mimi mwenyewe hapa mara chungu mzima nimeshakula mtu na rafiki yake , kawaida sana mbona, nadhani madem wanapenda mtu wanaemjua vzr kwa hio wanachukua shemeji. mwacheni penny she is like any other woman, alibugi kwa domo so kama ame learn something lets wait n c.
ReplyDeleteanony umenena, bongo hapa madem wanapenda kuchukuliana wanaume sana...yaani ukiwa na gf wako ukakaa na wenzake unaeza tomba wote within a week...na ndio wanaume wanavofanya siku hizi so watu wasimseme sana peny...atakuwa keshajifunza..
DeleteAcha movie liendeleeeeeeeeeeeeee
ReplyDeleteNyooooooooooooooo! Ovyo,
ReplyDeleteinavyoonyesha domo akitaka akutombe hata sasa hv ukatai!!! atawatomba sana na kuwaacha
ReplyDeleteNakuunga mkono mdau,misichana ya bongo inapenda maisha ya ready made.Ndio maana inaishia kudhalilishwa tafuteni mali zenu ma K nyie mkoje?
Deleteushamwagwa kaa kimya!
ReplyDeleteacheni ma2c jamani
ReplyDeleteKwikkw
ReplyDeleteU still cute don't let them play with your mind baby
ReplyDeleteNawashangaa mademu wa bongo wanashoboka nini kwa DOMO. Mtu mwenyewe Domo lake ka Mkundu wake! Mmamamamae zake!
ReplyDeleteNi kama ndrama ni kama video........endeleeeeeeni Wema akichoka Penny ingia hakuna shida tyme yenu itumieni.
ReplyDeleteDemu kaingia kitaa kaona maisha magumu sasa anaanza kupiga reverse.huku akijua mshikaji kwa kula matapishi ndio mwenyewe na kutegemea iko siku jamaa atarudi nyuma.
ReplyDeleteza saiz jaman
ReplyDeleteNi hivi Penny ulifanya kosa sana kumvulia chupi Diamond kwa 7bu ulikuwa ni shoga/udugu na Wema kama sitakosea.Hata kama ulikosana na Wema utakuwa bado we ni mkosaji kwani ulijua Diomond yuko vipi na shogayo wema.Hata kama waliachana wewe hukupaswa katu kumkubali Diomond kwa gharama yoyote ile ili kulinda heshima ya shogayo Wema ambapo nahisi Diomond aliwakuta mkiwa ni pete na chanda na wema.Kiuhalisia Diomond alikuwa na haja zake kwako tu na ameshazimaliza mwisho wa siku amerudi alikotoka na ww na wema sasa ni maadui hali ambayo 7bu yk ni wewe, kama usingemkubalia ushoga ungedumu, matokeo yake ss umejenga uadui na wawili wkt walikuwa ni marafiki kwako.Kwa kweli hapo ulibugi bora ungekuwa huna ushoga na wema.Ni akili gani ukubali umvulie nguo bwana/mume wa rafiki/jamaa/shoga/ndugu yako??? Ulitegemea nini?? Haya sasa yako wapi?? Hunae tena wema wala dio....
ReplyDeleteee ukome omalamimi atakae tembea nadia minamlogamana miminimemkuta yukopekeyake mimtoto watanga haaaaaaaatanga ikowp umeachwa nahauna bahati wenimbulula kamamm unavamiatu wemanadiamond huoni wanaendana kwnza ok malaunaonawivu akiwaanakmbatiwa namashabiki zakeweloho juu wapiwimwzi wamabwana umeachwa utakoma mama vp kigogo wapitena mamamkwe hajakutetea naulikua unajipendekeza wanawkewenzio ulkuaunatutia aibukujipendekeeza upendwe romama mwnamke hajpndkz kihvyo .
ReplyDeletepole ila n joo kwa nitkuffanya umshau dimond
ReplyDelete