RAISI UHURU KENYATTA WA KENYA AWASHANGAZA WENGI BAADA YA KUTEMBEA MJINI BILA MSAFARA WA WAWALINZI

Hii imetokea kwenye mji mkuu ambao ni Nairobi pale Rais Uhuru Kenyatta alipotumia gari moja tu bila msafara akitokea Ikulu kwenda kwenye hoteli moja kwa ajili ya kukutana  na Wanafamilia.
Unaambiwa toka amechukua madaraka, Rais Uhuru amekua na tabia hii mara kwa mara tofauti na Rais Kibaki ambae kila sehemu aliyotia mguu ni lazima aambatane na msafara hata kama ni maeneo ya karibu na Ikulu.
Askari mmoja wa usalama barabarani alipigwa butwaa pale alipojikuta kasimamisha gari ambalo ndani yupo Rais Uhuru bila msafara ambapo President mwenyewe alimwambia >>> “Ni mimi ofisa, fungua”. akimaanisha ni yeye amfungulie njia aendelee na safari.
Askari wa Usalama barabarani nchini Kenya wanasifia uongozi wa Rais Uhuru kwamba hata kukiwa na msafara huwa hawawekwi barabarani kwa muda mrefu kuusubiria upite manake wakati wa Mwai Kibaki ilikua inawalazimu wakae barabarani kwa saa kadhaa kabla ya msafara kupita.

Post a Comment

18 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kama umwema kwa raia wako kwanini uogope kutembea peke yako kama uhuru kenyata?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kweli..... Big Up Kenyatta.

      Delete
  2. alilidwa kuanzia akiwa mtoto maana alizaliwa ikulu.ameona mengi na ammejua yote ni ubatili.tatizo viongozi wengi wametokea kwenye familia za dhiki sana huko nyuma so wanafanya replacemnt.i lov u Uhuru

    ReplyDelete
  3. ni vizur ila asiishie hapo wakenya wanataka kuona mabadiliko chanya

    ReplyDelete
  4. Ni vyema lakini akumbuke yaliyomsibu Olof Palme wa Sweden.

    ReplyDelete
  5. Safi sana kenyatta na marais wengine afrika mashariki waige tabia hiyo. Mungu awe nawe

    ReplyDelete
  6. hawa ni kati ya wale wamtegemeao MUNGU na hakika hawatakwama achana na wale paranoids

    ReplyDelete
  7. Nataman ningekuwa hata mkenya..nchi yetu IMEOZAA..I wish turud tu kwenye ukoloni wa wazungu sababu huu wa watanzania unaudhii...kwi kwi kwi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kweli tumechoka na hii nchi ya ajabu.nataka niende ulaya

      Delete
  8. Safi kenyata sio wakina kikwete

    ReplyDelete
  9. Kutembea bila msafara sio dalili ya haki. Vp polisi wanaingia ktk majumba ya Ibada na kufanya kilichofanywa?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Naam umesema kweli,nchi yake yaongoza kwa mauji ya kionevu dhidi ya raia wasiokua ba hatia,ni juzi tu wameuwawa watu idadi isiojulikana ndani ya msikiti mombasa kwa kupigwa risasi na askari wa kenya. Kenya hakuna cha uadilifu wala nini,afadhali ya Tanzania mara 1000!!

      Delete
  10. uhuru kenyata amefata nyayo za obama safi sana marais kama hawa wanajielewa vizuri.

    ReplyDelete
  11. afanye haki Kwa wote sio upande mmoja

    ReplyDelete
  12. Wasi wasi wangu ni hao makafiri wa al-shabab ambao wapo katika kila kona ya Nairobi wasije waka mshababia.

    ReplyDelete
  13. Al shabab sio makafir unamjua kafir ww

    ReplyDelete
  14. eehhh Tunawajua, Wakristo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad