Mh. Tundu Lissu ameenda mbali na kusema, Mwl. Nyerere alizoea vya halamu na vya halali hakuviweza. Katika kuthibitisha maneno yake, Mh. Tundu Lissu alisema, mwaka 1968, Mwl. Nyerere aliudanganya ulimwengu pale aliposema kupitia gazeti la Observer la UK, “Iwapo umma wa Zanzibar bila ya ushawishi kutoka nje, na kwa sababu zao wenyewe, wataona kuwa Muungano una hasara kwa uhai wao, sitawapiga mabomu kuwalazimisha......Muungano utakuwa hauna tena sababu ya kuendelea iwapo washiriki wake wataamua kutathmini na kuthibitisha jambo hasa tukio la kihistoria kama Muungano'.
Mwaka 1984, Wazinzibari walipohoji Muungano, Alhaji Aboud Jumbe akafukuzwa kazi kwa amri ya Mwl. Nyerere na amewekwa kizuizini Mjimwema mpaka leo. Wolfgang Dourado akawekwa kizuizini, Bashiri Swanzy akapakiwa kwenye ndege ya kwanza akapelekwa Ghana.
Mh. Tundu Lissu aliendelea kusema, kwa vile Mwl. Nyerere alizoea vya kunyonga, kwenye Kitabu chake cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania, Mwl Nyerere alisema, 'huko nyuma baadhi ya viongozi wapinzani wa Muungano wameishawahi kusema tufanye referendum kwa Zanzibar kuhusu Muungano, tukakataa kwa sababu safi kabisa'.
Tundu Lissu anadai, Mwl. Nyerere hakukataa hoja ya Muungano kwa sababu safi kabisa, bali aliwaweka kizuizini wale waliohoji Muungano. Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uwongo na hakuweza kusema kweli.
Kitu muhimu kabisa cha kujiuliza na kufikiria. Kama kweli Mwl. Nyerere alikuwa anaishi kwa uwongo na udanganyifu, ina maana hata hati ya Muungano haipo na kama haipo, ina maana amewaingizwa 'mkenge' wananchi na hasa wanaCCM kwa kusimamia hoja ambayo kiuhalisia haipo. (Muungano wa serikali mbili).
Tukikubaliana na hoja ya Tundu Lissu, inabidi tujiulize, Kwa nini Baba wa Taifa alikuwa anaishi maisha ya uwongo na udanganyifu?. Alikuwa anafanya hivyo kwa manufaa ya nani?.
Kama hoja ya Tundu Lissu ni kweli basi hatuna budi kusema, kweli uwongo hupanda lifti wakati ukweli hutumia ngazi kuwafikia walengwa!.
Hoja hii inanipeleka kwenye angalizo la sababu ya baadhi ya wajumbe wakiongozwa na Leticia Nyerere kushauri bunge kwa nguvu zote liweke mipaka kwenye kanuni za bunge zikiwataka wabunge kutowadharirisha waasisi wa Muungano. Kumbe nyuma ya hoja zao walikuwa wanaogopa ukweli usijulikane!.
Mpaka katiba mpya ipatikane, tutaona na kusikia mengi!.
Kauli mbiu ni serikali moja au kila nchi ichukue fito zake kwa sababu watu tuliowatuma kwenda kumalizia mchakato wa katiba kwa sasa wanahoji uharali wa Muungano huku wakitaka mpaka makaratasi yenye sahihi za waasisi wa Muungano. Hawa wabunge wameshindwa kufanya kazi ya kumalizia mchakato wa Katiba badala yake wanaanza kuuliza kama Muungano ni halali au batili. Yaani baada ya Miaka karibia 50 ndiyo tunaanza kuuliza Muungano kama ni halali huku waasisi wa Muungano tukiwasema ni waongo na wadanganyifu.
Ninadhani kuna kitu hakiko sawa kwenye baadhi ya hoja za Wabunge!. ANGALIA VIDEO HAPA:
Hata kama tunataka serikali tatu, isifikie mahala tukamtukana mwasisi wetu kiasi hicho, ww tundu lisu una akili gan ya kujifananisha na Nyerere, nilikuwa nakuona unafaa kumbe hufai. madaraka tu. Hakuna nchi duniani inaweza kutukuna waasisi wake
ReplyDeleteHajamtukana bali,kamwambia kweli
DeleteHuyu tundu lissu hana akili yeye ana asila zake za chadena kuto kupata madaraka
ReplyDeletetatizi hata wenyewe si wakweli uongo kibao kama wangekuwa wakweli basi wasingedai serikali tatu kwa kuwa znz inaserikali yake basi wangesema na tanganyika pia iwe na serikali yake why wadai serikali tatu wakati hawana hoja za kuwashawishi wananchi akubaliane na serikali tatu? ni hivi waseme tu ukweli kuwa hatutaki muungano kwa kuwa tanganyika haina serikali yake kuliko kuendelea kuwadhalilisha waliotangulia mbele ya haki maana wangekuwepo hai haya yote yasingetokea
DeleteOvyo kabisa ... una haki gani kumshutumu Baba wa Taifa letu. Hakuna kiongozi alipenda uhai wa Tanzania kama Mwalimu. Ovyooo. Uwe unjifikiria kabla ya kutoa hoja. Kwanza kumuanaliz Mwalimu sicho kilichokupeleka bungeni . Ovyooo.
ReplyDeleteTundu lissu akapimwe akili.
ReplyDeleteIkifika stage ya kutukana aliyekufungulia mlango basi tena .
ReplyDeleteila kweli aka ka babu sikaelewi kabisa adi uwanja wa mpira kirumba akikipa chama.
ReplyDeleteAcha kumtukana baba wa taifa letu
ReplyDeleteMungu amlaze mahali pema peponi. Amina. Hajatukanwa baba wa taifa. Hoja ni kwamba kwa nn tume zote zilizokwisha undwa zinakuja na muundo wa serikali 3?
ReplyDeleteMungu amlaze mahali pema peponi. Amina. Hajatukanwa baba wa taifa. Hoja ni kwamba kwa nn tume zote zilizokwisha undwa zinakuja na muundo wa serikali 3?
ReplyDeleteMungu amlaze mahali pema peponi. Amina. Hajatukanwa baba wa taifa. Hoja ni kwamba kwa nn tume zote zilizokwisha undwa zinakuja na muundo wa serikali 3?
ReplyDeleteMalu'uni nyerere hajatukanwa bali tundu lisu amesema ukwli..huz ni zama za ukwli na uwaz nyny kaeni na ujinga wenu hamjui hata historiya ya nchi nyerere mnafiq
ReplyDeletesidhani kama Mhs Lissu alikuwa na nia ya kumtukana baba wa taifa, ila alikuwa na hoja nyingine ambazo zilikuwa zinahitaji ufafanuzi zaidi, au tu watu hawakumuelewa, hapa Tz hakuna kifaranga yeyote anayeweza kusema mabaya kuhusu Mwl. na hata kama alidanganya, lakini alidanganya kwa manufaa mazuri, EEh Mungu kwanza ahsante kwakutuletea Nyerere duniani, na tunaomba umlaze pema peponi.
ReplyDeleteuchu wa amdaraka tu hawa kina Lisu hawana lolote wanafikiri ikulu wataenda kwa kuwatusi waasisi wa taifa letu,Ashindwe na alegee katika jina la Tanzaniaaaaaaaaaaaaaaaaaaa,Tutakukumbuka na kukuenzi baba wa Taifa letu,Mungu ibariki Tanzania mungu ibariki Afrika na wasamehe hawa wasiojielewa
ReplyDeleteNyerere mungu wenuuuuuu mother fanta nyie
ReplyDeleteTunapenda kweli mawazo ya tundu lisu, ila kwa hili amekosea hakuna nchi yeyote duinian inadharau waasis wake, jembe tundu lisu naamin ulikuwa unasema hivo ili kutetea serikali tatu, omba msamaha kwa watanzania wote
ReplyDeletewTz vichwa vigumu kuelewa Lisu hapa kamsifu Mwalimu kw usani aliokuanao mana mpaka sasa watu wamuenzi kw usani wake wala hakua NABI,vipi asikoselewa na yy alikuwa mwana siasa kama wengine duniani Lisu ametoa hoja na ushahidi kuna waliofungwa mpaka sasa nakuna walio uliwa kosa la Lisu liko wapi? kaongea ukweli mtupu hatakama Mwalimu ni muhasisi lkn hoja alifanya makosa ama hakufanyaa????
ReplyDeletewTz vichwa vigumu kuelewa Lisu kamsifu Kambarage kw usani wake ambao mpaka sasa waenziwa,Kambarage hakuwa NABI alikua nimwana siasa kama wanasiasa wengine duniani vipi asikoselewe?Lisu katoa na ushahidi kuna watu mpaka leo wako gerezani kw ajili yakuficha ukweli na pia kuna walio uwawa hoja ya Lisu imeja ushahidi uliowazi sasa hapa amemtukana ama kaongea ukwelii??????
ReplyDeleteHajatukana mbona wambea wa kizee maana vizee ukiviambia ukweli utasikia Umenitukakanaaaaaa... kivipi yan nawe waambiwa ukweli?
ReplyDelete