UKAWA RUKSA KUFANYA MKUTANO ZANZIBAR LEO

Hatimaye mkutano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), uliokuwa umezuiwa kupisha sherehe za Muungano utafanyika leo katika Viwanja vya Kibandamaiti, Unguja baada ya kupata baraka za polisi.

Mkutano huo awali ulikuwa ufanyike Aprili 19, mwaka huu lakini ukazuiwa na polisi kwa maelezo kuwa intelijensia yao ilionyesha kuwa kungekuwa na tishio la maisha ya watu. Hivyo walishauriwa wapange tarehe nyingine baada ya Sikukuu ya Pasaka.

Hata Aprili 23 ambayo ilikuwa imepangwa kufanyika kwa mkutano huo, ilikataliwa na polisi kwa madai kwamba askari na maofisa wa jeshi hilo walikuwa Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano yaliyofanyika Aprili 26, mwaka huu.

Msemaji wa Polisi Zanzibar, Mohamed Mhina amethibitisha kuruhusiwa kwa mkutano huo na kuwataka wananchi watakaohudhuria kuwa watulivu kabla na baada ya mkutano.

“Tumewaruhusu kufanya mkutano huo lakini maandamano hayataruhusiwa kufanyika,” alisema Mhina.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Julius Mtatiro alisema mkutano huo utakaoanza saa 8 mchana hadi saa 12 jioni, utahudhuriwa na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF, Freeman Mbowe na Dk Willibrod Slaa wa Chadema, Mchungaji Christopher Mtikila wa DP na Dk Emmanuel Makaidi wa NLD.

Wengine ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, wawakilishi 10 kutoka kundi la 201 na wanachama mbalimbali kutoka umoja huo.

“Tunakwenda kuwaelimisha wananchi nini maana ya Katiba, jinsi ya kulinda maoni yao waliyoyatoa yasichakachuliwe na kuwaeleza kwa nini tuliamua kutoka bungeni,” alisema Mtatiro na kuongeza:

“Kesho (leo) tunafanya mkutano Unguja na keshokutwa (kesho) Pemba na tutatoa ratiba ya mikutano mbalimbali itakayofanyika Tanzania Bara kwa makundi tofauti.” Aprili 16 mwaka huu, Ukawa wakiongozwa na Profesa Lipumba walisusia Bunge la Katiba na kutoka nje kwa madai ya kutokuridhishwa na mienendo ya mjadala ya Bunge hilo.

Baada ya kutoka bungeni, walitangaza kufanya mikutano nchi nzima wakianzia Zanzibar.
Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Replies
    1. Sema umewachoka mkundu wewe!tumewachoka na nan?

      Delete
  2. UKAWA MBONA MNATAKA KUCHEZA NA AKILI ZA WATANZANIA HII KURA YA MAONI INA MAANA GANI MMEKAA KAMA SI WASOMI MNGEKAA BUNGE MKATUNGA KATIBA MWISHO SISI TUTAIHUKUMU TU TUNASIKIA NA KUONA SASA HUKU MITAANI MNATAKA NINI NYINYI AU MNATAKA ROHO ZA WATU ILI MRUDI
    BUNGENI NA HOJA NZURI KWA KUTUMIA ROHO ZA WATU KAMA MNAINGIA MITAANI BASI KURA YA MAONI ISIWEPO KAMA NDIO HIVYO SISI TUNATAKA KUKUONENI MKIJENGA HOJA BUNGENI SIO MITAANI MBONA HAMJIAMINI WANANCHI WAPO NA WATAIHUKUMU KATIBA IKIWA HAIFAI NYINYI KAZI YENU IPO BUNGENI MSITUMIE SIASA VIBAYA HILI NI SUALA LA KITAIFA MNAWEZA KUITIA NCHI MATATIZONI KAMA VIPI WACHENI WANANCHI WAAMUE KITU WANACHOKITAKA KAMA MAONI YAO YATAKUA HAYAJASIKILIZWA BAC WATAIHUKUMU NYINYI KATUNGE PUMBA AU NZURI BUNGENI TUACHIENI TUAMUE HIZI SI KAMPENI ZA KISIASA TUACHENI HURU WANASIASA TUPATE KUKUPIMENI

    ReplyDelete
  3. boss kama hujui nyamaza hapo juu .tunaisaport ukawa kwa sababu wanataka rasimu iloyopelekwa ya tume ndio ijadiliwe sasa kule bungeni ukisema hayo unaambulia matusi sasa ni haki yao kuwaeleza wananchi kwann walitoka na kwann wameamua kususia mpaka leo ni haki yao sasa kama ww hupendi usiwafuatilie

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yap muelimishe huyo mkuu umefanya la maana sana kuna watu kama hawa huwa hawajui a wala be wapo wapo tu kazi kulaumu upinzan kwa mambo muhimu wanayopigania kutujuza sisi watu wa chin!inasikitisha kuona mtu kama huyu nae anawalaumu Ukawa na wakat akiona hali halisi ya mchakato inavyochakachuliwa hiv watu kama hawa huwa hamuon hata picha basi kama kusoma hamjui?

      Delete
    2. Safi mkuu mweleze huyo jamaa maana kuna watu vichwa tikiti maji kabisa wew husom magazet au maana unaona kila siku hao mafisad wanataka kuchakachua katiba then na wew bado unawasaport unaakil au ndio matope.

      Delete
  4. Hongeren ukawa mko juu

    ReplyDelete
  5. Mwambie huyo mpe elimu afahamu

    ReplyDelete
  6. Wananchi wenyewe wamekunywa maji ya bendera ya ccm wanajisumbua labda karume na nyerer wa fufuke ndio watafanikiwa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad