Ligi kuu ya Uingereza imeendelea tena jioni ya leo kwa mchezo kati ya Manchester United dhidi ya timu iliyopanda daraja ya Leicester City.
Man United ambao walishinda mechi iliyopita ya ligi dhidi ya QPR kwa ushindi wa magoli 4-0, leo hii wameonja kipigo kizito kutoka kwa Leicester, baada ya kukubali kufungwa 5-3.
Man United ndio waliokuwa wa kwanza kuliona lango la Leicester kupitia Robin van Persie, kabla ya dakika baadae Angel di Maria kuongeza la pili.
Dakika moja baada ya United kufunga goli la pili, Leicester wakafungw goli la
Kwanza kupitia Ulloa na mpaka mapumziko matokeo yalikuwa 2-1.
Kipindi cha pili Ander Hererra akaifungia Man United goli la 3, lakini dakika chache baadae Leicester wakapata penati na kufunga goli la pili, huku United wakiwa bado na hasira za kulalamikia maamuzi ya refa, Estaban Cambiasso akafunga goli la kusawazisha.
Mchezaji aliyeng’ara kwenye mchezo Jamie Vard akaifungia City goli la 4, kabla ya dakika baadae Nugent kufunga goli la tano kwa mkwaju wa penati.
Mpaka refa anapuliza kipenga cha mwisho Leicester City 5-3 Man United.