Nimfanye Nini Huyu Mdada wa Kazi?

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

Nina mdada wa kazi kuna siku kwa bahati mbaya alinikuta uchi chumbani.

Story yenyewe ilikuwa ivi: Nilitoka kuoga kumbe yeye alikuwa chumbani anachukua nguo za kuvaa watoto shule, sasa mie sikumuona vizuri nikajua tu ni wife kumbe ni yeye, basi kwa kujiachia nilikuwa nimeweka taulo mabegani na uku chini nikiwa mtupu manake yeye alikuwa upande wa pili wa kioo, sina ili na lile kumbe yeye na alishajua mie niko pale na kusema alishindwa kabisa kuwa nijifunike ili yeye apite, badala yake akaamua kupita ivyo ivyo na kuanza kusema samahani mara kaniamkia uku akipita nyuma yangu mikiwa sina ata chupi. 

Mi kuona vile na sikuwa na la kufanya nikaamua kumuangalia tu na sikusema chochote.

Basi tangia siku ile kitu nilichokiona ni kama anataka kulipa fadhila za kuuona uchi wangu manake mara anakaa mapaja wazi , mara anajifanya amelala uku sehemu ya mwili wote wa mapaja ikiwa wazi uku akiwacha sehemu ya mlango wa chumbani kwake wazi ili nami nimuone na anafanya ivyo wakati wife hayupo nyumbani.

Sasa wadau mitihani imekuwa mingi akijikosha kwa alilolifanya na kwa kweli sijamwambia wife kuhusu lile tukio lote, ni mimi na yeye tu tunaojua. 

Naombeni ushauri wadau nimfanye nini uyu dada wa kazi manake sasa vituko vimezidi nyumbani manake ni kama mtu anataka kuweka mambo sawa kwa kuwa ameniona nikiwa mtupu nae anataka mi nimuone vile vile.
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Chukulia kama hajakuona kabisa ulikua unaota tu, nadhani hii itasaidia kutoleta mifarakano katika ndoa yako, vilevile acha kumtazama kwa uoga, simama kama baba na ikibidi umkemee ikiwa ataendelea na mikao yake ya ajabu. Nafikiri kwa leo inatosha lakini akirudia uje tena kusema hapa nitakupa njia nyingine.

    ReplyDelete
  2. wewe ni baba. na baba siku zote anatakiwa awe na msimamo ili familia yake isiyumbe. Ukilala na huyo msichana inamaanisha kwamba unataka familia yako isiwe na lepe la heshima, kwanza hatakuheshimu wewe, pili hatamuheshimu mkeo na tatu atataka kuwafanya watoto kama amewazaa yeye namaanisha kuwa yeye ndie mwenye kutawala na si mkeo. Ushauri wangu kwako mkemee mbele ya mkeo na tena muulize mkeo akiwepo kama mkeo sio mtu wa kupanik.kama ni mtu wa kupanic mkanye wewe mwenyewe huyo dada ili akuogope. pia tabia gani ya kuingia chumbani kwa wazazi hata kama mmeamuru aingie chumbani kwenu anatakiwa awe anagonga chumbani kwa sababu naamini kipindi anakuja kuchukua ngua alijua kwamba wewe upo na si mkeo ndio maana alijitawala lakini angekuwepo mkeo wala asingeingia bila hodi

    ReplyDelete
  3. Ulitakiwa umkemee alipoingia tu chumbani maana inaonekana hakugonga mlango, maana angegonga ungejua sio mke wako. Mkemee kwa anayoyafanya ataacha na usimuendekeze

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad