Baada ya timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Star’ kulazimishwa sare ya kufungana magoli 2-2 na Algeria kwenye uwanja wa taifa, kocha mkuu wa kikosi hicho Charles Boniface Mkwasa amesema, mabadiliko yaliyofanywa na benchi la ufundi kumtoa Elius Maguli na kumingiza Mrisho Ngassa hayakuzaa matunda kama walivyotarajia.
Mkwasa amesema, walimuanziasha Maguli kwasababu ni mchezaji ambaye anatumia nguvu na anaweza kupambana kwa kutumia mwili wake lakini baadaye walimpumzisha wakiamini kuingia kwa Ngassa kungeifanya timu kutengeneza nafasi nyingi zaidi za kufunga kwasanbabu Ngassa anaspidi na uwezo wa kutengeneza nafasi.
“Niseme tu kwamba leo (jana) ilikuwa ni game yetu 100% tumetengeneza nafasi nyingi sana lakini tumeshindwa kuzitumia tumepata goli mbili lakini kuna muda tumepoteza concentration wakaweza kurudisha goli zote mbili lakini vijana wamepambana wamehangaika kutafuta magoli kutokana na nafaisi zilizopatikana na wakati mwingine tunasema mpira unabahati na Algeria wanabahati sana”, alisema Mkwasa.
“Vijana wamejitahidi lakini niseme tulifanya makosa pengine wakati wa kufanya mabadiliko kwasababu timu ilishakuwa stable lakini ni matokeo ya mchezo na nafikiri bado tunamlima mrefu kwasababu ninavyowatazama hawa nyumbani kwao watabadilika. Lakini uwezo wa kuwafunga tunao timu yao sio nzuri sana kiasi kwamba haifungiki”.
“Niwashukuru watanzania na waandishi wa habari kwa kuhamasisha na watanzania wameweza kuitikia na tumeona jinsi gani wameishangilia timu yao lakini wasife moyo kwa matokeo haya, tupo katika mchakato wa kujenga timu naamini katika muda mfupi tutakuwa na timu nzuri kama wenzetu ambavyo wanatimu zao”.
“Niwashukuru pia wachezaji na wengine wote ambao tumeshirikiana, kamati pamoja na TFF kwa kuweza kuonesha kiwango ambacho kwa muda mrefu hakijaonekana”.
Kikosi cha Stars kimeondoka jana usiku kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa marudiano utakaopigwa Jumanne November 17.
Mliweza kuiba Kura ibeni Na Magoli sasa, wapelekeni wakatalii Algeria wasiopafahamu warabu waahamaliza kazi.
ReplyDeleteUMELEWA?AU UGONJWA WA AKILI UNAKUANZA?
DeleteBado mna-weweseka eeh!, uchaguzi umeisha bro- CCM mbele kwa mbele
Deletetusife moyo mkwasa?sikuelewi.wewe ni mtaalamu-tactician -unapokiri kwamba ulifanya makosa,basi uelewe huko ndio kushindwa.upepo wa ushindi kwa matumizi ya uwanja wa nyumbani siku zote unasimamia asilimia tisini ie 90%.algiers au tangies sijui mtachezea uwanja upi muwapo algeria nafasi ya ushindi ni ile ile asilimia 10 tuu kwa 90 ya algeria.sasa boniface mkwasa unaiharibu dhamana yako nzito kwa watanzania kwa kuthubutu kuvuruga team,kuvuruga upangaji,kuharibu pattern.mnagharimiwa mno stars,tena mno.mimi naona baada ya algeria urudi yanga chini ya kocha mkuu,wewe kuwa kocha mkuu majanga.
ReplyDeletearudi ruvu stars.kitu kimoja tuelewe,kazi ya team coach kubwa kulio zote ni kuwapanga wachezaji walio bora katika kikosi bila upendeleo, kuendelea kuusoma mchezo,kupima morali na mwelekeo wa kiuchezaji,kuwapanga wachezaji hususani washambuliaji kutekeleza uwanjani mbinu-magoli yasiyotegemewa katika kuutafuta ushindi.kubadili wachezaji ovyo-ovyo ni hatari na uhuni,anakushangaa unayemwita nje na anakushangaa pia unayemwingiza kuchukua nafasi yake.makocha wetu bado, mnalilia kazi,mnapewa,mnawaangusha wananchi yaani zero-zero pumba-mashudu.hufai mkwasa.
ReplyDelete