Breaking News: Kigogo wa BOT Azuiwa Airport Kutokana na Kukosa Vibali vya Kusafiri nje ya Nchi

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Kigogo mmoja mzito wa Benki kuu ya Tanzania (BoT) amezuiwa kusafiri kwenda nje ya nchi yeyey na familia yake kutokana na zuio lilipo kwa sasa kwa watumishi wote wa umma.

Kigogo huyo alikutwa na songombingo hilo baada ya kufika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere (JNIA)kwa minajiri ya kwenda nje ya nchi kwenda kula bata na familia yake wakati huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka (Xmass na mwaka mpya). Kigogo alidai kuwa safari hiyo alikuwa kagaramikia yeye
mwenyewe kwa pesa yake , wala siyo ya serikali, ila waksema kuwa kwa sasa kuna pini ya kwenda nje
ya nchi kwa mtumishi wa umma .

Kigogo huyo alihojiwa katika chumba maalumu na maofisa wa uhamiaji kwa muda wa kutosha lakini majibu yake yalionekana kujikanganya na kukosa msingi, hivyo aliamrishwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha hapo uwanjani kabla ya kutumbuliwa jipu kama wale wanne wa TAKUKURU walivyotumbuliwa.

Source: Citizen
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hii habari imekaa kidaku daku
    rais kazuia safari za kikazi zisizokuwa na ulazima
    sasa huyu anasafiri kimpango wake na familia yake
    mgemtaja basi huyo kigogo
    hii habari ya uzushii

    ReplyDelete
  2. pini hiyo, alikuwa anakimbia nchi huyo akijua yeye ni jipu lijalo!

    ReplyDelete
  3. Kama kwa pesa yake kwanini atoloke wasijue asipoelekea angekaa asubiri sheria fisadi uyooo

    ReplyDelete
  4. Wanakimbilia nje kuweka mambo sawa katika account zao za nje. Hakuna kutoka mtu mpaka tupate repoti ya account zenu huko nje. JPJM alisema wametuibia kiasi cha kutosha, wametuchakachua kiasi cha kutosha, SASA BASI, NA BASI KWELI.
    Mlisema mpo tayari kwa mabadiliko, hakuna kuishi kwa mazoea........HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  5. Tuwe waangalifu na maamuzi mengine
    Watendaji msiige kila kitu
    Fanyeni kazi kwa ungalifu
    Yasije token kama samaki wa Magufuli

    ReplyDelete
  6. Hii sasa ishakuwa kuwa shida labda ana marafiki zake au ndugu tuuishio ughaibuni
    Tusinyanyasane kiasi kwa kulipiza kisasi
    Samaki WA mafuguli walitocost meli ilikaa miaka uliza kiasi gani tulilipa mbona hamsemi
    Magufuli kasema Safari za kikazi hata kama zimeghalimiwa na wafadili lazima Kibali toka ikulu, Kama ni kuzuia hata kikwete basi mzuueni tujuwe nani kalipa gharama za Safari hii pamoja Na walinzi wake

    ReplyDelete
  7. labda alikuwa anatoroka kijanja!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad