Kuna Double Standard Kwenye 'Utumbuaji Majipu?'

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Kuna wengine wanapewa grace period ya siku 7 kurudisha fedHa walizojiatia kwa kukwepa kodi. Waliopitiliza siku 7 mpaka sasa hatujasikia wakimulikwa na kamera za Waandishi wa Habari kama ilivyo kwa wengine na kuswekwa ndani!

Wakati wengine wakitenguliwa vyeo vyao kwa kutotimiza wajibu wao ipasavyo kiukweli ni kwamba Idara zote za Serikali zimeprove failure kama tutafuata Standard ya Magufuli strictly.

Mathalani ajali za barabarani zimezidi sana hasa mwisho wa mwaka lakini hatuoni kama hili ni "jipu" kwa Magufuli! "Jipu" ni wale akina mama wanaolala chini Muhimbili!

Kama Magufuli atataka kutenda haki ashughulikie pia wanasiasa waliowasababisha watendaji chini yao kutotimiza wajibu wao! Ajue kabisa tatizo halikuwa kwa watendaji, bali "wazee wa vimemo" ndo waliotufikisha hapo!
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kuna double standard ya kupongeza yale mazuri yaliofanywa na muheshimiwa Magufuli kwa kipindi kifupi kabisa? Hata Mwenyezi Mungu alipoiumba hii dunia hakuiumba kwa siku moja. Na hata alipomaliza kuiumba ilichukuwa muda kukamilika kwa vitu vingine hadi kuitwa dunia tunayoiona hivi sasa. Kwa hivyo tuache maswali ya kifisadi, raisi apewe ushirikiano na muda wa kufanya kazi yake kwani aliyokwisha kuyafanya ni makubwa ukilinganisha umri wa uraisi wake. Watanzania majungu yasiokuwa na mshiko yanayoambatana na siasa za majitaka ndio dili kwetu. Na ndiyo yalioifikisha nchi yetu pabaya hapa ilipo. Sasa leo katokezea kiongozi anaepambana kuondoa ufisadi na kuishi kwa mfumo wa ujanja ujanja na wizi miongoni mwa watanzania kunatokezea watu wanaojifanya wakosoaji na kujifanya wanajua zaidi lakini kiukweli ni wanafiki wasioitakia mema nchi hii.

    ReplyDelete
  2. Kamati kuu ya CCM ndo tatizo hapa

    ReplyDelete
  3. watanzania kwa kukosoa hatujambo haya hata angeshuka malaika tungemkosoa
    long live JPJM

    ReplyDelete
  4. Kwakweli Anony 6:30 Mungu akubariki sana tena sana kwa majibu yko mazuri sana umetujibia watanzania wengi wenye mapenzi n.a. uzalendo wa kweli kwa nchi yetu aijalishi me ni ukawa lakini ukweli utabaki ukweli tu Rais wetu ni Mungu katuzawadia hasa cc wanyonge. Sasa tulikuwa upinzani tukijiita wanyonge tumepata mtetezi wa wanyonge tunakosa hata roho ya kushukuru. Hivi huyo mtoa mada ni Mtanzania kweli au?! Umenikera Nahic n wewe ni miongoni mwa majibu yaliyotufikisha hapa Leo. Kama huna cha kuandika bora ukae kimya tena nakusisitizia kaa kimya fisadi mkubwa we we. kwa sasa watu tunajivunia kuzaliwa Tanzania,tutolee siasa zako za uvundo hapa. nakuomba baba Mungu wa mbinguni mlinde rais wetu mpendwa mh MAGUFULI asijeambukizwa mijipu ya mafisadi mapapa wakati akizidi kuyatumbua .

    ReplyDelete
  5. Ni kweli kabisa vimemo vinatutesa hasa watumishi wa chini, hawa mawaziri wenyewe wanatoa tu amri sijasikia wakiongea na watumishi japo kubaini hata changamoto zinazowakabili na kupelekea wkt mwingine kazi kuzorota, wao wanajifanyia suprise tu. MH. MAGUFULI mwenzenu alitembea karibu nchi nzima amebaini changamoto wanazopata watumishi wa vyeo vya chini pamoja na wananchi kutotendewa haki aidha na wanasiasa au wakurugenzi ndio maana unaona anatumbua tu majipu kwa urahisi kwa sababu ameshajua wapi yameota. Nina wasiwasi viongozi bado hawajaielewa kauli mbiu ya HAPA KAZI TU. tupunguze vimemo tufanye kazi vinginevyo tatizo la urasimu halitaisha milele

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad