Zoezi la uwekaji alama nyekundu katika zaidi ya nyumba 100 zinazotakiwa kubomolewa kwenye bonde la Mto Msimbazi, Jangwani limemalizika chini ya ulinzi mkali wa polisi baada ya vurugu za wananchi kuigomea serikali katika zoezi hilo.
Zoezi hilo lililoanza leo majira ya saa nne asubuhi likiongozwa na Mwanasheria wa NEMC, Machare Heche lilisababisha vurugu zilizotokana na wananchi kukataa kuwekewa alama hizo huku wakidai kuwa zoezi hilo alikustahili kufanyika kutokana na kusimamishwa kwa zoezi hilo hadi Januari mosi mwakani.
Alipohitajika kuzungumzia zoezi hilo kwakuwa alikuwepo wakati tukio zima hadi kumalizika kwakwe, Heche aligoma kuzungumzia zoezi hilo kwa kudai kuwa mzungumzaji mkuu ni Waziri anayehusika na Mazingira, January Makamba au Mkurugenzi wa NEMC.
Miongoni mwa malalamiko ya wananchi waishio katika bonde hilo ni kutaka jengo la Stendi ya mabasi yaendayo haraka pia liwekewe alama na hatimaye kubomolewa kwa sababu ya kuwa jengo hilo lipo bondeni sawa na nyumba zao,
Aidha wameiomba serikali kuongeza siku zaidi za maandalizi ili waweze kuhamisha vitu vya majumbani kwani muda uliotolewa hautoshi kufanya maandalizi.
Ikumbukwe kuwa zoezi la kubomoa nyumba zilizopo mabondeni lilianza Desemba 17 mwaka huu na kusitishwa baada ya siku tatu na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi hadi Januari 5 kwa kigezo cha kutoa nafasi kwa watu waliojenga katika maeneo hayo kuondoa wenyewe mali zao .
Nyumba 100 Zawekwa X Jangwani, Vurugu Zatawala
6
December 30, 2015
Tags
poleni sana,inauma sana. lakini hamna jinsi, majipu lazima yakamuliwe.
ReplyDeleteMajipu ni lazima yakamuliwe bila kujali ukubwa na mahali jipu lilipokaa. Haya mazoeamazoea ya Watanzania kufanya vitu kwa kufuata njia za panya ndio yamelifikisha hili Taifa hapa lilipo. Kila Mafuriko yanapotokea na Watu wanapopoteza maisha unakuta Rais mzima na Mkuu wake wa Mkoa wanaenda kuwajulia hali ya kuwapa pole badala ya kuwaambia ukweli wa adhari za kujenga kwenye mabonde na kuchukua hatua stahiki. Hili liwe fundisho kwa baadhi ya Watanzania ambao wamezoea kuendesha maisha yao kiujanja ujanja.
ReplyDeleteacheni kuongea pumba hayajawakuta kuna watu kinondoni mkwajuni nyumba zimebomolewa na zipo mahali salama hakuna mafuriko
ReplyDeleteKwani hakuna chombo kikubwa kabisa cha kisheria ambacho hawa watu wanaweza kwenda kuishtaki serikali kwa ukatili inao wafanyia wananchi wake! mbona IPTL ilipoona hapa tz haijapewa haki ikaenda ngazi za kimataifa na wakapewa haki ya kulipwa mabilioni ya shilingi hadi wakazigawa kwa mafisadi wa serikalini! na nyinyi jiungeni mwende mahakama ya kimataifa ili mjue kama serikali ipo sawa au la!! mkumbuke hata bhakhresa alisha kwenda na akalipwa iliyokuwa kamata.
ReplyDeleteJAMANI HAPO KAZI TU, WAMEAMBIWA SIKU NYINGI, LAKINI WOTE VIZIWI AJABU WENGINE BADO WAMEJENGA MWAKA JANA ,BAADA TU YA MAFURIKOM YA MWE<I APRIL MWAKA JANA WATU WAMEFYATUA TOFALI NA KUANZA UJENXI SASA NYINYI MNAFIKIRI SEREKALI IFANYEJE NA HAKUNA HATA MTU MMOJA MWENYE KIBALI CHA KUJENGA (BUILDING PERMIT)
ReplyDeleteTUMUOMBE MUNGU LAKINI NI SHERIA WALA MAGUFULI ASILAUMIWE HIO KAULI KAIKUTA IPO KAMAILIVYO YEYE ANATEKELEZA TU. WARUDI KWO VIJIJINI KWANI WENGI WAO NI WAGENI TIKA MIKOANI WAMEFIKA NA KUVAMIA TU
Kwanza kabisa napenda kuanzia na kusema maeneo mengi ya wazi nchini yalivamiwa kwa baraka za CCM
ReplyDeleteWanainchi walianza na kufunguwa matawi ya wakelekwetwa wa CCM viongozi wakuu wa ccm walifunguwa matawi haya kwa vishindo
Watu wa kaanza kujenga sehemu hizi hasa Jangwani Dar , yakawa ni mazoea mafuriko yakitokea missada inatoka serikali ya ccm ikawa inatumia mabilion ya fedha , Tanzania tuna sehem kubwa sana ya watu kuuishi sasa kwanini wasitengeze maandalizi kwa watu hawa?
Kabla , Kama ni uvamizi ccm ni namba moja maeneo mangapi nchini yalikuwa wazi CCM imejenga ofisi zao.
Nafikiriki hata hayo mahekalu ni kulipiza kisasi tu ,
Yatawagharimu sana haya ccm