Wema Sepetu Amuingiza Mkenge Mwanamuziki Diamond Platnumz....

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
MAPYA tena! Baada ya hivi karibuni staa wa Bongo, Wema Sepetu kuuvaa msala wa kudaiwa kutumia maji na umeme kwa wizi, madai mazito yameibuka kuwa, wizi huo ulikuwa ukifanyika tangu alipokuwa na nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Ijumaa ‘Kubwa’ linatambaa nao.

Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho kipo karibu na Diamond, baada ya Wema kubanwa na wafanyakazi wa Tanesco na Dawasa akidaiwa kutumia huduma hizo ‘kimazabe’ na kwamba ni kwa miaka kadhaa, Diamond alishtuka kwani anavyojua yeye walikuwa wakitumia maji na umeme kwa malipo sahihi.

SIKIA MWENYEWE
“Taarifa kwamba Wema alikuwa akitumia maji na umeme kwa muda mrefu bila kulipia imemshangaza sana Diamond. Anachosema ni kwamba, Wema kamuingiza mkenge kwani wakati wako pamoja (kimapenzi) alikuwa akitoa pesa kwa ajili ya kulipia huduma hizo.

Hata hao wanaosema kwamba, Diamond aliujua mchezo huo wanamuonea maana alikuwa akitoa
mkwanja kwa ajili ya chakula, maji na hata umeme. Sasa kusikia kwamba wakati anaishi pale na Wema huduma hizo hazikuwa zikilipwa ameshangaa sana,” alisema rafiki huyo wa Diamond na kuongeza:


Hata hivyo, Diamond mwenyewe hataki kuongelea suala hilo kwa kuwa uhusiano wao ulishaisha licha ya kwamba anasisitiza kuwa, kama kweli halipii umeme na maji tangu enzi za penzi lao, kamuingiza mkenge kupitiliza.” Baada ya kuzipata taarifa hizo, mwandishi wetu alimtafuta Wema kwa njia ya simu ili kujua kama kweli deni analodaiwa la maji na umeme ni la tangu akiwa na Diamond, lakini simu yake haikuweza kupatikana hewani.

DIAMOND HUYU HAPA
Alipotafutwa Diamond kuzungumzia sakata hilo alisema kuwa, yeye na Wema walishaachana hivyo kuanza kumzungumzia haiwezi kuleta picha nzuri. “Nikiwa pale kwa Wema nilikuwa kama mshua, nilikuwa natoa mkwanja kwa ajili ya matumizi ya msosi, maji na hata umeme sasa kama yametokea hayo
kwamba alikuwa akitumia huduma hizo bure, mimi siwezi kuongelea hayo,” alisema Diamond.

TUJIKUMBUSHE
Wiki mbili zilizopita, Wema alikwaa msala wa kudaiwa kutumia umeme kwa kuchezesha mita. Kikosi kazi toka Tanesco, kilivamia nyumbani kwake, Makumbusho na kukata umeme ikidaiwa anadaiwa pesa nyingi ambazo hazikuwekwa wazi. Siku tatu mbele, jamaa wa Dawasa nao walimfanyia ‘ziara’ ya kushtukiza na kumkuta na kosa la kutumia maji huku akiwa amegeuza mita hali inayomwingiza katika wateja wanaoonekana kuibia taasisi hiyo. Wakasema deni analodaiwa mlimbwende huyo ni shilingi milioni tisa (9,000,000).
GPL
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kweli udaku huu

    ReplyDelete
  2. mnauhakika na Magazeti. acheni unafiki hata mawairi wanaiba serikalini iatakuwa Maji na umeme

    ReplyDelete
  3. MBONA WENGI WANAIBA? SASA WEMA IMEKUWA NYIMBO YA TAIFA. HATA HAO WANAOANDIKA NAO WIZI TUU.

    ReplyDelete
  4. Dai asijishaue bure, alikuwa anatoa sh. ngapi na familia yake ilikuwa inaishi kwa Wema. Angalie Ivan kaenda white part yeye kabaki kuchunga chumba cha kizee cha ug.

    ReplyDelete
  5. jamani part ya Zari vepeeee. x Ivan ndo kalipia kila kitu Domo kala kona

    ReplyDelete
  6. 2:56 ulikuwepo alipolipia kila kitu mbona roho yako mbaya hivyo kwa uongo utakufa Mdomo upande

    ReplyDelete
  7. Tatizo d anaishi kwa ajili ya watu. See now anavyojidharirisha ili watu wajue yako OK Na z. Huyo demu mtamboo utakufa kishujaa chunga kijana mdudu every where.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad