Kikosi cha Polisi cha Wanamaji Kimekamata Shehena ya Mizigo Isiyolipiwa Kodi Bandarini DSM

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

Kikosi cha Polisi cha wanamaji kimekamata jahazi likiwa linatokea bandari ya Zanzibar kwenda bandari ya Dar es Salaam likiwa limesheheni bidhaa mbalimbali zikiwemo spika za redio na friji wakati jahazi hilo liliondoka bandari ya Zazibar kibali chake kikionyesha kuwa limebeba mafuta ya marashi.

Ripota wetu alifika makao makuu ya kikosi hicho na kukuta jahazi hilo linaloitwa Najat likiwa limejaa vifaa hivyo huku polisi na wafanyakazi wa jahazi hilo wakisaidia kushushwa kwa vifaa hivyo ambapo kamanda wa kikosi hicho Semboje Kanga amesema nyaraka za mzigo haziendani na kilichobebwa

Katika hatua nyingine wenye mzigo huo wamejitokeza na kusema kuwa wananyaraka zote muhimu na wanashindwa kuelewa kwa nini polisi wanasema shehena hiyo wanamashaka nayo.

 

Naye mliki wa chombo hicho kilichokamatwa Bw Iddy Hadibu amesema kilichotokea ni kwamba wakati wanakuja bandari ya Dar es Salaam baharini wakakuta chombo kingine kimelemewa na mzigo na ndio wakawasaidia ili wasipate shida na hapo ndipo walipojikuta wanaingia katika dhahama hiyo.
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Habari zenu sometimes mizinguo kweli kweli ni sawa na mtu alievaa kiatu cha kushoto kwenye mguu wa kulia na kiatu cha mguu wa kulia akakivaa kwenye mguu wa kushoto fresh vichunguzwe hivyo vyeti vyenu fake vya uandishi wa habari kama kweli mlifaulu kihalali kwenye fani hiyo ya uandishi

    ReplyDelete
  2. Nakuunga mkonono Mdau hawajui hat kueleza ukaelewa hawa pia majipu

    ReplyDelete
  3. Mbona Alichoandika ndio kimeonyeshwa leo na ITV??

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad