Mama Diamond Afanya Kufuru...Akarabati Nyumba Kwa Mil 100 na Kununua Mtaa Mzima

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

KUFURU! Mama wa staa mwenye jina kubwa Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kasimu ‘Sandra’ amedaiwa kufanya kufuru ya aina yake kwa kununua mtaa mzima, Tandale-Uzuri jijini Dar na kuikarabati nyumba yake aliyokuwa akiishi zamani kwa kutumia takriban shilingi 100 Milioni

Chanzo chetu makini ambacho kilifuatilia ishu nzima tangu nyumba hiyo ilipoanza kukarabatiwa, kimesema kwamba kwa kipindi kirefu ‘bi mkubwa’ huyo amekuwa akifika nyumbani hapo asubuhi na kuondoka jioni akisimamia ujenzi sambamba na binti yake, Esma.


 Nyumba hiyo kabla ya kukarabatiwa.


“Mama Diamond noma, kateketeza shilingi milioni 100 na bado nasikia ameshafanya mchakato wa kununua nyumba za jirani ili mtaa mzima uwe wao,” kilisema chanzo chetu.

Chanzo hicho kimezidi kutiririka kuwa mama Diamond anataka kuifanya nyumba hiyo kuwa bora zaidi kwani mbali na kuiboresha, kuna mpango wa kutengenezwa swimming pool (bwana la kuogelea).

 Ikiwa inakarabatiwa


Mara baada ya kupenyezewa ubuyu huo, gazeti hili lilifika kwenye nyumba hiyo na kuzungumza na mama Diamond aliyekuwa bize kusimamia ujenzi.



“Jamani! Taarifa hizi mmezitoa wapi tena? Kweli nimekarabati nyumba yetu iwe bora zaidi. Hayo mambo ya gharama na mipango mingine ni siri labda mje mmuulize Diamond akirudi Marekani lakini ukarabati huu mnaouona ndio nimeusimamia mimi na mwanangu Esma,” alisema mama Diamond.
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kwa uongo tuu hamjambo.

    ReplyDelete
  2. KIKI + UBISHOO = DNA

    ReplyDelete
    Replies
    1. kweli wewe ni masikini kafiri, utajibeba

      Delete
  3. Muundo wa nyumba zenu zote ni wa aina moja kuanzia rangi na madirisha mpka rangi za mapaa...halafu kwa utajiri huo wakununua mtaa mzima si mumoe kazi mkandarasi nyie akimaliza mje mkague nyumba hahahah eti tunanunua mtaa mfyuuuuu

    ReplyDelete
  4. Nyie udaku acheni kuuza mambo mbona kawaida tu kufanyia ukarabati nyumba

    ReplyDelete
  5. kufanya ukarabati ndo kununua mtaa mzima? Ulimbukeni hautoki kwenye damu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad