Mbunge Vicky Kamata Afunga Ndoa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Likwelile

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Mbunge wa Viti Maalamu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Vicky Kamata amefunga ndoa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Servacius Likwelile.

Dk Likwelile amefunga ndoa hiyo baada ya mkewe wa awali kufariki dunia Mei mwaka 2014.

Kwa hatua hiyo, Dk Likwelile amemfuta machozi mbunge huyo kijana baada ya ndoa yake ya awali aliyotarajia kuifunga na Charles Pai kukwama dakika za mwisho wakati wa maandalizi yote ya msingi kukamilika.
Dk. Likwelile


Habari ambazo Tanzania Daima imezipata, zilieleza kwamba mbunge huyo ambaye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya , alifunga ndoa hiyo Septemba mwaka jana katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Geita.

Habari zinaeleza kuwa wawili hao baada ya kufunga ndoa, hawakuwa na sherehe kubwa bali walikuwa na ‘pati mchapalo’ iliyofanyika nyumbani kwa Dk Likwelile na kuwashirikisha baadhi ya wana ndugu na marafiki wa pande zote mbili.

“Wamefunga ndoa bomani, hakukuwa na sherehe bali kulikuwa na hafla ndogo iliyofanyika nyumbani na wanafamilia wachache ndio walioshiriki,” alisema mtoa habari wetu ambaye alikuwa mmoja wa watu wachache walioshuhudia ndoa hiyo.

Alipotafutwa kwa njia ya simu kuthibitisha taarifa hizi, Kamata alikiri kufunga ndoa hiyo, lakini hakuwa tayari kuzungumza zaidi.

“Umepata wapi hizi taarifa? Ila ni kweli nimefunga ndoa, ninachojua ni kwamba Dokta Likwelile ni mume wangu halali, namshukuru Mungu kwa hilo,” alisema kwa kifupi Vick na kukata simu.

Mei 24 mwaka 2014, Vick Kamata alikwama kufunga ndoa na Charles Pai baada ya kubainika kuwapo kwa kasoro kwenye nyaraka za mwanaume.

Hali hiyo ilisababisha mbunge kuugua ghafla kutokana na mshituko alioupata na kulazimika kulazwa katika Hospitali ya Tabata Genaral iliyopo Segerea. Ndoa hiyo ilikuwa ifungwe katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mkombozi, Sinza jijini Dar es Salaam na tayari kadi za mialiko zilikuwa zimesambazwa kwa watu mbalimbali wakiwamo wabunge.

Kamata ni msanii wa muziki aliyetamba na kibao chake cha “ Wanawake na Maendeleo” na pia ni mtetezi wa haki za wanawake.
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mbona mmeweka picha ya balozi Sefue??,

    ReplyDelete
  2. Huyo Dr hata Mwaka haujafika kasha oa duuu

    ReplyDelete
  3. HUYU VICKY ANA MATATIZO YA AKILI. SIO KWELI KWAMBA AMEOLEWA NA DR LIKWELILE. HIVI WEWE VICKY UNA MATATIZO GANI KULAZIMISHIA NDOA WNANUME HAWAKUTAKI UNAWALAZIMISHA? YULE ALIYEKUTOROKA DAKIKA ZA MWISHO HAJAKUPA SOMO BADO? MWANAUME KAMA ANAKUPENDA ATASEMA YEYE SIO WEWE UKIMBILIE VYOMBO VYA HABARI KUTANGAZA. HAKUNA UBAYA KATIKA KUOLEWA LAKINI SIO KWA MTINDO HUU WA KUONGOPA ETI UMEFUTWA MACHOZI. MWNAMKE HUNA HAYA KWELI WEWE. JAMANI HAJAOLEWA HUYU ANATAFUTA KIKI. POLE WE!

    ReplyDelete
  4. Vicky ana kila kitu is ipokuwa mume. Hilo linampa wazimu ndio maana anasingizia kuolewa.hajaolewa chochote anajaribu kujipendekeza aolewe. Kuolewa bahati Vicky na hupangwa na Mungu. Kama hujaandikiwa usilazimishe.unatumia nguvu nyingi na zaidi unamchafua tu baba wa watu. Tulia Mungu atakupa mume usilazimishe.

    ReplyDelete
  5. ACHA USANII WEWE UNAVYOPENDA NDOA HALAFU ETI UFUNGE KIMYAKIMYA?DANGANYA TOTO

    ReplyDelete
  6. mwongoo tena anapenda ndoa za hadharan kasahau aliliwa na yule msela mamaeeee...atupishe kwanza anakula bure mapesa mengi kwa ajiri ya .................................. hakuna cha ndoa wala nini sisi tupo geita na anaefungisha ndoa tunamjua hakuna cheti chake na wala kwenye orother hayupo kwenye kitabu awadanganye wapumbavu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad