Mwanafunzi wa darasa la saba Shule ya Msingi Laela A, Ruti Sikapitaamefariki dunia baada ya wazazi wake kukataa kumpeleka hospitali kwamadai kuwa imani ya dhehebu lao haliruhusu waumini wake kutibiwa hospitali.
Tukio hilo lilitokea Machi 17 baada ya mtoto huyo kuugua kwa siku tatu
huku akiwa anafungiwa ndani na baba yake Cossam Sikapita, akidai kuwa
hawataki aende hospitali kupatiwa matibabu kwani kwa kufanya hivyo angekuwa ametenda dhambi kwani dini hairuhusu kutibiwa na dawa za hospitali.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Laela, Didas Simtengui,alisema kuwa mtoto
huyo alikuwa anaumwa kwa siku tatu na hawakumpeleka hospitali badala
yake walikuwa wanazidisha maombi wakiamini kuwa atapona.
Mmoja wa majirani, Musa Mwanakulya alisema kuwa wao walikuwa hawamuoni
mtoto huyo akienda shuleni na wenzake na walijua anaumwa na ametibiwa
isipo kuwa maombi ni kitu cha kawaida na walikuwa wakisikia wanaomba
kila siku katika nyumba hiyo.
‘’tulikuwa tunasikia wakisali sana huku wakiwa wamejifungia ndani,
tulipo uliza walidai kuwa wanamuombea Ruti anaumwa lakini hawataki
kumpeleka hospitali wakidai kuwa mafundisho ya dini yao haya ruhusu
kutibiwa hospitali….waliendelea kumuombea mpaka akafariki
dunia’’…alisema.
Majirani walipopata taarifa kuwa mtoto huyo amefariki kutokana na wazazi wake kugoma kumpeleka hospitali, walikwenda kuvamia katika nyumba hiyo
wakitaka wawakamate wazazi hao ili nao wawaue.
Kutokana na vurugu kubwa kuibuka ililazimu polisi wa kituo cha Laela
wafike katika eneo hilo na kuwatawanya watu waliokuwa na hasira kali
na kuuchukua mwili wa marehemu kwenda kuuhifadhi katika chumba cha
kuhifadhia maiti kilichopo katika kituo cha afya cha Laela na wazazi
wa mtoto huyo kuwaweka rumande ili kuwaokoa na wananchi wenye hasira
kali.
Mtoto Afariki Kwa Kukosa Matibabu..Wazazi Waliamini Maombi Pekee
0
March 21, 2016
Tags