TBC1 Hawana Pesa ya Kurusha Bunge ila Wana Pesa ya Kumrusha Paul Makonda

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Jana nikiwa nyumbani naperuzi peruzi channel zetu zina nini cha mimi kuweza kuangalia, wakati napitapita nikapita na TBC, chaneli yetu ya Taifa. Nakutana na Makonda anahutubia, akili ya mwanzo nikawaza labda Rais Magufuli yuko sehemu na Makonda kaalikwa.

Baadae inapita banner kuwa ni kikao cha Makonda na watendaji wa Halmashauri, dah kinarushwa live televisheni ya taifa. Nadhani tatizo lililopo TBC ni aidha kukosa priorities au kuleta siasa lakini si rasilimali fedha au kubana matumizi kama wanavyotuaminisha.
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Acha uchuro wewe mwandishi, kikao cha makonda cha siku moja tena masaa tu unaweza kufananisha na vikao vya bunge vya muda mrefu? Tunataka maendeleo na maendeleo hayaji kwa kufuja mali ni lazima ubane matumizi ili kupiga hatua vinginevyo maendeleo tutayasikia na kuyaona kwa wenzetu tu.

    ReplyDelete
  2. Makonda Kama mkuu mkoa wa Daresalam sio mtu wa kubeza . He is the head of state's executive branch of the government.kwa maana ya kwamba makonda ndie raisi wa dar licha yakuwa haja pigiwa kura na wananchi lakini ameteuliwa na mkuu wa nchi aliepata idhini kutoka kwa watanzania ya kuwaongoza na makonda anapata baraka hizo kwa kuteuliwa na muheshimiwa raisi ili awe mwakilishi wake wa serikali yake kwa ngazi ya mkoa kwa hivyo bila ya kutafuna maneno muheshimiwa Makonda ni raisi Dar pena usipende na chochote kitakacho tokea Dar kina muhusu muheshimiwa Makonda kwanza kabla ya kumfikia muheshimiwa raisi wa nchi.Na kutokana na kuwa vyombo vya habari vyingi kuwepo mkoa wa daresalam hapana shaka vyombo hivyo vina wajibu wao wa kutoa ushirikiano wao katika shughuli za kikazi kwa muheshimiwa wao wa mkoa.

    ReplyDelete
  3. Mwandishi ni jipu hajui asemalo wala aindikalo

    ReplyDelete
  4. Maoni finyu? Bunge ni chombo cha kutunga sheria na mbunge ni mwakilishi wa wananchi bungeni kuwasilisha maoni yao kwa serikali kuu. Mkuu wa mkoa ni mwakilishi mkuu wa serikali kwa wananchi mkoani na msimazi mkuu wa masuala yote ya mkoa.mbunge anaweza kuchukua matatizo ya wananchi na kuyawasilisha serikali kuu lakini mwisho wa siku ni mkuu wa mkoa atakaekuwa na dhamana ya kuhakikisha mkoa wake mzima unapiga hatua ya maendeleo. Mbunge ni mwakilishi wa ni jimbo lake tu utaona tofauti hapa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad