Watu Wasio Julikana Wasambaza Vipeperushi vya vitisho Visiwani Zanzibar

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Siku moja kabla ya kufika siku ya uchaguzi mkuu wa marudio visiwani Zanzibar hapo kesho watu wasio julikana usiku wa kuamkia leo wameziwaekea X Nyekundu nyumba kadhaa za wakazi wa Pujini katika wilaya chake chake chake na kuwaekea kipeperushi cha onyo juu ya ushiriki wao kwenye uchaguzi huo.

Moja kati ya watu walio wekewa X hizo kwenye  nyumba yake amesema wamelala walipo amka walijikuta nyumba zao zikiwa tayari zina X na kuekewa kipeperushi hicho cha onyo.

Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa Kusini Pemba ilifika kijijini Pujini Kumvini na Kijili kujionea nyumba hizo zilizo wekewa X nyekundu ampapo mwenyekiti wakamati hiyo mkuu wa mkoa Kusini Pemba Bio Mwanajuma Majidi Abdalla amewataka watu wanao taka kwenda kupiga kura waende kupiga kura na kuzipuzia X hizo huku ulinzi ukiwa umeimarishwa.

Bimwana Juma amewataka wanaume wasiwatishe wana wake kwa kutishia talaka kwa sababu ya kwenda kupiga kura badala yake wawape uhuru wanawake kuamua pindi wakitaka kwenda kwenye uchaguzi waende pasi vitisho vya vua aina yoyote.

Nae kamanda wa polisi mkoa kusini pemba kamishimna msaidi mohamed shekhan mohamed amesema jeshi lake halitishiki na vitendo vya aina hio na kwamba watawakamata wale wote waliohisika na uwekaji wa x hizo.
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Muwakamate mnawajua au ndo nataka kubbikia watu kesi ili mkawatese...mishenzi hii cjui lini itawacha kunyanyasa waja wenzao.lol

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad