Hivi Ndivyo Irene Uwoya Alivyojifungua Kwa Upasuaji Bila Ganzi

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Msanii wa filamu Irene Uwoya amesema hakupenda kabisa kujifungua kwa upasuaji lakini ilimbidi afanye hivyo ili kuokoa maisha yake pamoja naya mwanaye.

Muigizaji huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwae Krish, amekiambia kipindi cha Uhondo cha EFM kuwa wakati anaelekea hospitali kucheki afya yake na maendeleo ya mimba yake, hakujua kama ndio siku ambayo angejifungua kwa kuwa hakuwa na dalili yoyote.

“Kwanza nilikuwa sipo Tanzania, nilikuwa na siku moja toka nirudi, so kesho yake nikaenda hospitali kuangalia mimba inaendeleaje. Kiukweli namshukuru Mungu sikuwahi kusikia maumivu ya uchungu, nikaenda pale Regency, kwa hiyo dokta kuniangalia tu akasema mtoto anachungulia wewe unatembeaje?, nikamwambia mimi sijui na hapo nimevaa kiatu kirefu kweli, akaniambia toa viatu mtoto anachungulia,” alisimulia Irene.

“Wakanifanyia vipimo, lakini baadaye wakaniambia huwezi kujifungua kawaida, njia ndogo kwa hiyo inabidi tukufanyie upasuaji. Kiukweli nilitamani kujifungua kawaida. Lakini nikikumbuka ile siku nakumbuka kile chumba kilivyotisha, kitu ambacho nakumbuka sana ni ganzi, walikuwa kila wakipiga inakataa, ikabidi nifanyiwe upasuaji hivyo hivyo, yaani nilipata maumivu makali mpaka nikawa naweweseka nahisi niko Paris kwa sababu kila walichokuwa wanakifanya nilikuwa nakisikia,” aliongeza Irene.

DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL BLOG HAPA
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ganzi inakataa kwa sababu damuni kuna amount kuabwa ya alcohol ndo maana mtu anapata ajali kalewa ndii hapati matibabu mpka pombe iishe unampaje ganzi mtu ana pombe kibao mwilini hawezi kusikia ganz...ila pole irene duuuh mm niliongezewa njia tu sikupigwa ganzi lakn nilisikia kuzimia kwa maumivu ya kushonwa na kuchanwa jamn sikien tu hv vitu

    ReplyDelete
  2. mjifunze kwenda hospital za serikali! hiyo waliyokuchoma haikuwa ganzi.!

    ReplyDelete
  3. wewe Irene kwa nini ulikuwa unakunywa sana pombe ukiwa mjamzito na inaelekea ulikuwa unafakamia sana pombe mkapa ganzi kukataa, ushukuru mwenyezi mungu kuwa mtoto alizaliwa akiwa salama, sababu ukiwa unakunywa sana pombe mtoto huwa anazaliwa akiwa na matatizo, mimi mwenyewe nilikunywa pombe siku moja halafu jino likaniuma nikaenda kwa mganga wa meno apanipiga sindano ya ganzi moja tu ikashika kabla aanze kutengeneza jino, inaelekea nilikuwa sinywi sana pombe labda kiasi tu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad