Madhehebu ya Kiislam Yafunguka Kuunga Mkono Kasi ya Rais Magufuli na Utumbuaji Majipu Uchungu...

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
KASI  ya Rais, Dkt. John Pombe Magufuli inazidi kushika moto baada ya Kiongozi Mkuu wa Chuo cha Kiislam (Hawza) Imam Swadiq ambaye pia ni Kiongozi Mkuu wa Waislam wa Madhehebu ya Shia Ithnasheria, Tanzania,  Shekh Hemed Jalala amewataka Watanzania na waumini wa madhehebu yote nchini kumuunga mkono kwa kasi yake.

Shehe Jalala akizungumza leo na wanahabari katika maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mmoja wa  wanafunzi wa Mtume Mohamed (S.A.W),  Imam Ali (A.S), amesema alikuwa kiongozi jasiri, mpenda haki,  aliyepinga rushwa, muwajibikaji na mpinga ufisadi, kama ilivyo kwa sasa kwa Rais Magufuli ambaye ameonesha nia ya dhati ya kuifanya Tanzania kuwa mpya kwa kupinga ufisadi, rushwa  na mambo mengine ambayo yanawaumiza Watanzania wa hali ya chini.
“Tunaadhimisha zaidi ya miaka  1430 ya kuzaliwa kwake

Imam Ali kwa kuwa alikuwa mwanafunzi bora wa kuigwa kwa kile alichokipigania ndicho kinachoonekana kwa Rais Magufuli, viongozi wa dini tuwaongoze waumini wetu katika kumuombea na kukemea pale tunapoona si sahihi, ila mpaka hapa tulipo ameonesha dira ya Tanzania mpya,” alisema Shehe Jalala.
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad