Msanii Ali Kiba Amkana Tena Jokate Adai sio Wapenzi na Kufunguka Makubwa....

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Msanii Ali Kiba amefunguka kuhusu suala la ndoa na mwanamitindo maarufu hapa Bongo Jokate Mwegelo, ambaye inasemekana yupo naye kwenye mahusiano ingawa mwenyewe anakanusha.

Akiongea kwenye kipindi cha eNews kinachorushwa na East Africa Television, Ali Kiba amesema siku hizi watu wanasahau na kudharau waliyokuwa wakiyafanya wazee wetu katika kuchagua mke wa kuoa.

“Unajua siku hizi watu wanasahau kuwa wazee wetu walikuwa wanachagua vipi msichana, siku hizi tunaoana tu, unaishi nae miaka mitatu, lazima muwe marafiki, hivyo ni vigumu kuachana na rafiki, ila ni rahsi kuachana na mpenzi wako”, alisema Ali Kiba.

Pia ameendelea kusisitiza kuwa yeye na Jokate ni marafiki tu na sio wapenzi kama watu wengi wanavyodhani na kuibua maswali yenye utata kuhusu kauli yake ya kwanza aliposema "Unapooa, lazima muwe marafiki na huyo mwandani wako, ili kudumisha ndoa yenu".
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad