Najuta Kuachana na Mke Wangu wa Kwanza – Gardiner

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Mtangazaji wa Clouds FM, Gardiner G Habash amesema miongoni mwa vitu anavyojutia katika maisha yake ni kuachana na mke wa kwanza aliyezaa naye mtoto wa kike, Karen, ambaye kwa sasa yupo mwaka wa pili chuoni.

Akiongea kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV, Gardiner alisema kutokana na kubadilisha kazi ya awali na kuwa mfanyabiashara kipindi anaishi Mwanza, alijikuta akiiweka kwenye mawe ndoa yake kwa kukosa muda nayo.

“Yale mazingira niliyokutana nayo Mwanza ya kibiashara yalisababisha nikaachana na mke wangu wa kwanza, ni kitu ambacho najuta,”alisema staa huyo. “Nisije nikasema sana mwisho nikalia hapa bure,” alisisitiza.

Amesema mke wake huyo kwa sasa aliolewa japo wana mawasiliano mazuri sababu ya mtoto wao. Kuhusu kama anajuta kuachana na Lady Jaydee, Gardiner alisema: Siwezi kusema najuta kwamba alitokea kwenye maisha yangu na siwezi kusema kwamba najuta tuliachana. Lakini ninachoweza kusema tu kwamba kwa suala la Jaydee ni suala ambalo nilichagua sana lisiwe ni jambo ambalo nalizungumzia au kulitolea comment kwasababu yule ni public figure unaposema kitu kuhusu yeye tafsiri zinakuwa ni tofauti na vile unavyotarajia.”

“Kwahiyo sina majuto yoyote, na sina aina yoyote ya chuki au uadui na nategemea hata yeye atakuwa anafeel the same,” alisisitiza.

Alidai kuwa yeye na Lady Jaydee hawana mawasiliano ya aina yoyote kwa sasa na mara ya mwisho walikutana kipindi wanakamilisha taratibu za talaka.

Kwa upande mwingine Gardiner amedai kuwa maisha aliyonayo sasa ni ya furaha tele. Mtangazaji huyo amejiunga tena na Clouds FM akitokea EFM.

Bongo5
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Acha ungese wewe mzee g habash na utazurula sana kuajiriwa wakati wadogo zako wanakaribia kufungua radio zao au ndio ndi ndi ndi!!!! milembe inakuhusu.

    ReplyDelete
  2. nadhani kama una mtoto yupo mwaka wa pili chuo wewe tayari ni babu so achana na malumbano yasiyo na msingi kama taraka ulishapewa na majuto siku zote ni mjukuu kaa chini ujipange upya kama kuoa oa utulize boli.

    ReplyDelete
  3. I don't blame you sana G, after all the marriage between the two of you ( Jide) was so fake from the beginning.You left your first wife because of Jide, always remember "malipo ni hapa hapa duniani" Jide alikuwa anamtukana mke wako kwa message and you never reacted so you see now. I blame Jide because he is the reason why you could not show full love to your daughter. And bad enough she thinks what she did to your wife will remain unpaid! No. Jide ujue ulichukua mume wa mtu usijifanye eti wewe mwema na G mbaya na wewe ndio sababu ya mtoto wa G kuishi bila baba, baraka ya hiyo ndoa ingetoka wapi??? Mungu anaona kila kitu.

    ReplyDelete
  4. What happened to you will be a lesson to all nyumba ndogo zinazovunja ndoa za watu na kuolewa wakifikiri kuna baraka zozote toka kwa Mungu. Ndoa ni mpango wa Mungu na kama kuna hila yoyote basi ujue haitadumu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad