Machangudoa Waja Juu Wataka Biashara yao Ita

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

Baadhi ya wanawake wanaojiuza katika mitaa ya Majengo B na Fisi, mjini Mpanda mkoani Katavi wameitaka Serikali kuandaa utaratibu wa kuwatambua ili nao waweze kulipa kodi na kuliingizia taifa pato kutokana na shughuli wanayofanya ya kuuza miili yao.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana usiku, baadhi yawanawake hao walisema wanafanya kazi kama zilivyo kazi nyingine kwani zinawaingizia kipato kizuri kinachowasaidia kutimiza mahitaji yao ya msingi hivyo kazi hiyo inapaswa kuheshimiwa na kutambuliwa na serikali.


Mmoja wa wanawake hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Joyce, alisema ni wazi Serikali ikiandaa utaratibu mzuri wa kuwatambua itawafanya waweze kulipa kodi ambayo italiongezea pato taifa tofauti na ilivyo sasa ambapo wamekuwa hawalipi kodi kwa kuwa hawatambuliwi.


" Sisi kazi yetu ina kipato kizuri kutokana na makubaliano yanayofanyika kati na wateja wetu lakini Serikali haitaki kututambua hivyo sio rahisi hata kututaka tulipe kodi, nchi nyingine watu kama sisi tumetambuliwa na tunalipa kodi serikalini" alisema Rosemary Kazeze.


Aliongeza kwamba kipindi hiki ambacho Serikali inatafakari au haioni umuhimu wa wao kutolipa kodi, anawashauri kina dada poa wenzake kuacha tabia ya kukwepa kwenda Nyumba za kulala wageni zinazotambuliwa na Serikali kwani kufanya  hivyo kunaikosesha serikali mapato


Alisema kuwa siku za nyuma walikuwa wanafanya biashara hiyo katika madanguro kitendo ambacho polisi walikuwa wakiwasumbua kwa kuwakamata kutokana na misako ya mara kwa mara, lakini hivi sasa hawasumbuliwi kwani wamepanga vyumba katika gesti halali na wanalipia vyumba hivyo na mmiliki analipa kodi kwa msingi huo nao wanachangia pato la taifa.


“ Kaka yangu mwandishi tunashukuru sana hata wewe kutufikia, wanatudharau na kutunyanyasa sisi lakini wateja wetu wakubwa ni hao hao viongozi wa serikali na tasisi nyingine lakini wajue kufanya biashara ya ukahaba sio sababu ya kuto muunga mkono Rais wetu katika suala la mapato ya serikali”…alisema Mayasa Hussein
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hatutaka mapato ya laani, watafute tafsiri ya kazi watajua kuwa ukahaba haipo katika kazi halali zinazotambuliwa na serikali yetu. Aibu yao ikae na hela zao na laana yao pia.

    ReplyDelete
  2. Hata sisi WANAUME tunaitaka biashara hii iwe halali tuna wateja kibao si wanaume si wanawake

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mhh wee mbona uweleweki, unasema hata nyinyi wanaume mnaitaka kazi hiii, na mnawateja kibao si wanaume si wanawake hebu pambambanua vizuri, yakwamba upo kundi gani? Wasomaji tupate kukuelewa

      Delete
  3. kweli dunia imekwisha mnataka mtambulike kwa umalaya wenu? washenzi wakubwa hapa sio ulaya ni Africa, si bora muwe ma house maid kuliko huo pumbavu wenu, hamtatambulika hadi kiama

    ReplyDelete
    Replies
    1. "Do what your thought wilt".............sky is not the limit!!

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad