Nimegundua Wanawake wengi (85%) Wanateseka Sana Ndani ya Ndoa....Embu Zindukeni.....

Hili jambo limeniuma sana tena sana, wanawake wengi wanaonewa na waume zao bila kusema popote wakijua ndio kuvumilia kumbe hawajui wanajiua pasipo kujua inaniuma sana.

Nimeongea nawanawake zaidi ya 20 walio wengi hawana raha ya ndoa au tuseme tuu ya maisha wanasema wanavumilia huku miaka inaenda wakiwa ndani ya mateso makali, Kama kulea familia wenyewe bila kusaidiwa na baba hata senti, kufungiwa nje bila huruma yani kufukuzwa, kutukanwa na kudharauliwa, kupigwapigwa hivyo hata kuachiwa ulemavu, kubebeshwa mzigo wa kulea watoto wenyewe au kutelekezewa watoto mwanaume akapotea kabisa nyumbani baada ya miaka kumi hadi ishirini ndio anarudi na watoto wanamfurahia bila mama kufanya lolote, wanaume 98% kutokuwa waaminifu ndani ya ndoa zao, kuambukizwa magonjwa ya zinaa na ukimwi, na kugeuzwa kuwa punda wake bila huruma, kwakweli hili jambo limeniuma sana wanaume walio wengi ni mashetani wanaigiza kuwa binadamu hivyo kupelekea wana wake kufa haraka.

Wanawake embu zindukeni kuna maisha zaidi ya ndoa, msikubali kufa mapema kisa neno ndoa yapo maisha zaidi ya ndoa bana msikubali kunyanyaswa hata kidogo yapo maisha bila mume na yenye amani msikubali utumwa nikujitengenezea kifo chakujitakia.

Hii ni rai kwa wanawake wote walio ndani ya ndoa nawale wanaotarajia kujiunga na ndoa, ndoa sio mateso, ndoa sio msalaba, ndoa sio uvumilivu wala ndoa sio lazima.
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sidhani kama mwandishi umetumia akili katika andiko lako hili???
    nahofia ulikuwa unahoji makahaba waliopata mimba kiholela mtaani wakashindwa hata kumjua baba wa mtoto.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama wewe ndoa yako iko vizuri mshukuru Mungu kimya kimya usikufuru

      Delete
  2. Mengi sana yana ukweli, ila mnapokuja kwenye hizi percents, naona mnakurupuka tu kama nanihii..

    ReplyDelete
  3. Wewe uliyo comment hapo juu,,,Mungu akusamehe maana hujui yliandikalo ila Imba Mungu yasikukute

    ReplyDelete
  4. Ndoa za kiafrika wengi walioolewa(wanawake)ni sawa na vile wapo utumwani wao ni watu wa kumenyeka daily kupika kufua kufanya usafi wa mazingira kuzaa na kulea watoto mwanaume amekaa tu ukimuuliza eti mimi ndiyo mfanya kazi naleta hela ya kula na mavazi it doesn't make any sense mimi nilidhani ulimuoa mkeo kwa kumpenda kumbe nyuma yake ulikuwa unatafuta mtumwa wa kukuhudumia na kukuzalia watoto duh!noma ndiyo maana ndoa siku hizi mabinti wengi hawana mzuka nazo kwa mifano walioiona kwa mama zao lazima watu muende na wakati hii siyo karne ya stone age ukiuliza utaambiwa ni mila na desturi what?Mila gani hizo za kumfanya binadamu mwenzako mtumwa?huyo huyo kuna siku unamgeuza punching bag sasa hayo ndiyo mapenzi?Huu ni wakati mwingine lazima twende na wakati kabla ya kumuoa ulikuwa unamtoa sana out ulipomleta ndani tu ni komeo out unaenda mwenyewe na unarudi home time yeyote ile unayoitaka eti kwa kuwa wewe ni mume haupaswi kuulizwa maswali na mkeo umeishasahau ulivyoapa siku unamuoa huyo mtumwa wa kike yaani ndoa zetu ni bomu kinoma zina ukatili wa kijinsia wa hali ya juu inatakiwa tubadilike iwe 50/50 na si vinginevyo la sivyo hizo siku za usoni kutakuwa kitu chq kuitwa ndoa ni hadimu sana

    ReplyDelete
  5. Ndoa za kiafrika wengi walioolewa(wanawake)ni sawa na vile wapo utumwani wao ni watu wa kumenyeka daily kupika kufua kufanya usafi wa mazingira kuzaa na kulea watoto mwanaume amekaa tu ukimuuliza eti mimi ndiyo mfanya kazi naleta hela ya kula na mavazi it doesn't make any sense mimi nilidhani ulimuoa mkeo kwa kumpenda kumbe nyuma yake ulikuwa unatafuta mtumwa wa kukuhudumia na kukuzalia watoto duh!noma ndiyo maana ndoa siku hizi mabinti wengi hawana mzuka nazo kwa mifano walioiona kwa mama zao lazima watu muende na wakati hii siyo karne ya stone age ukiuliza utaambiwa ni mila na desturi what?Mila gani hizo za kumfanya binadamu mwenzako mtumwa?huyo huyo kuna siku unamgeuza punching bag sasa hayo ndiyo mapenzi?Huu ni wakati mwingine lazima twende na wakati kabla ya kumuoa ulikuwa unamtoa sana out ulipomleta ndani tu ni komeo out unaenda mwenyewe na unarudi home time yeyote ile unayoitaka eti kwa kuwa wewe ni mume haupaswi kuulizwa maswali na mkeo umeishasahau ulivyoapa siku unamuoa huyo mtumwa wa kike yaani ndoa zetu ni bomu kinoma zina ukatili wa kijinsia wa hali ya juu inatakiwa tubadilike iwe 50/50 na si vinginevyo la sivyo hizo siku za usoni kutakuwa kitu chq kuitwa ndoa ni hadimu sana

    ReplyDelete
  6. Hizo asilimia naona zimekosewa lakini kuna ukweli juu ya mateso ya wanawake kwenye ndoa. Pia ametoa point nzuri kwamba kuna maisha nje ya ndoa.

    Kitu cha msingi ni mwanamke kujitegemea kiuchumi ndio ataweza kujitegemea kimaamuzi. Pia kujua kuwa kumwacha mwanaume mtesaji si kitu cha aibu bali ni kujikomboa. Mateso yanatoka na hali kwamba nikimwacha huyu mwanaume nitakula nini au Jamii itanionaje. Wito: Wanawake tafuteni kipato chenu muwe na nguvu ya kujitegemea. Pili ondoeni aibu.. ndoa mbaya ni kifo. Ondokeni na kuanza maisha mazuri bila ndoa.

    Wanaume malaya, wasiotunza familia hawastaili mwanamke mwema na msiwape nafasi waacheni watangetange.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad