Wabunge wa UKAWA, Bakini Bungeni Mlisaidie Taifa

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Nawaomba kwa ujumla wenu. Najua hamuivi na Naibu Spika kwa mnavyomlalamikia. Najua kuwa mmeshatangaza kutoka kila Naibu Spika anapoliongoza Bunge na mmekuwa mkitoka kweli. Najua mna malalamiko yenye mashiko. Najua mnalilia ulinzi na ustawi wa demokrasia ndani na nje ya Bunge.

Kesho,mjadala wa Bajeti utaanza. Naamini,wakosoaji ndiyo wafuatiliaji na wasomaji. Wasomaji wa nyaraka kwa haraka na baraka Bungeni ni Wabunge wa Upinzani. Ni Wabunge wa UKAWA. Wabunge wa CCM hupumbazwa na uchama na wingi wao.

Msipokuwepo kesho na kuendelea,Wabunge wa CCM hawataijadili Bajeti. Wataisifu;kuisifu Serikali; kumsifu Rais na Naibu Spika na kuiunga mkono bajeti kwa asilimia mia. Bajeti itakosa kuchambuliwa na kukosolewa. Bajeti ni moyo wa nchi. Isipowekwa sawa,wote tutaumia. 

Tafadhalini,Wabunge wa UKAWA bakini Bungeni muifinyange bajeti ya nchi. Fanyeni hivyo kwa kulisaidia Taifa. Msijali yatakayosemwa kuhusu kubaki kwenu Bungeni!

Mzee Tupatupa-Kilaza wa Lumumba,Dar es Sal
_________

LOVE STORY YA UTANIKUMBUKA NEYLA Ipo tayari ni maandishi na Sauti !, Kuisoma yote Bonyeza HAPA Lipia tsh 1000 Tu mtandao wowote,au Tembelea www.makapedia.com

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. uliandika hili huna akili kabisa

    ReplyDelete
  2. hivi mbowe pale usoni alipigwa ngumi au nijuze mwandishi uliyeposti hiyo picha

    ReplyDelete
  3. HAPO NDIYO TUTAUJUA UZALENDO WAO NA MASILAHI YAO JUU YA TAIFA LETU. LAIVU NOT LAIVU!

    ReplyDelete
  4. Mbowe na Lipumba wana vipara sasa ni wakati wa kung‘etuka mtoke kwenye madaraka muwape vijana,mawazo yenu ni ya kizamani,acheni kushkilia madaraka,na vipara vyenu.Mzee Msimbazy

    ReplyDelete

Top Post Ad