Polisi Wavamia Nyumbani Kwa Diamond Platnumz Usiku...

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Polisi wenye silaha hivi karibuni wali ka nyumbani kwa msanii nyota, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anayeishi Mivumoni Madale na kusitisha shughuli za burudani zilizokuwa zikiendelea ndani, Risasi Mchanganyiko limedokezwa.

Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, shughuli iliyositishwa  na polisi ilikuwa ni ile ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mama mzazi wa mkali huyo wa muziki, Sanura Kassim ‘Sandra’ iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. Ilidaiwa kwamba msanii huyo amekuwa akifanya sherehe mara kwa mara katika nyumba yake hiyo, hali inayosababisha kero kwa baadhi ya majirani zake, ambao nao, wamekuwa wakilalamika mara kwa mara kwa viongozi wa serikali ya mtaa huo.

Gazeti hili baada ya kuupata ubuyu huo, lilifunga safari hadi nyumbani kwa msanii huyo na ku kia ofisini kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mivumoni, Deodatus Kamugisha ambaye baada ya kuulizwa kuhusu kuwepo kwa tukio hilo la askari kuzima sherehe hiyo, alikiri kuwa ni kweli.

“Nimekuwa nikipata malalamiko ya mara kwa mara kuhusu sherehe za Diamond kuwa waalikwa wake ni vijana wa kihuni ambao wakija huwa wanavuta bangi hadharani, wanafunga barabara pamoja na kujisaidia haja ndogo hovyohovyo maeneo ya nje ya nyumba yake.

“Juzi nilipigiwa simu usiku na majirani zaidi ya sita wakila lamika kuhusu sauti kubwa ya muziki wa kwenye sherehe ya Diamond, nilimuita lakini akakaidi, ikabidi niende Kituo cha Polisi cha Wazo na kuchukua polisi wakiwa na silaha na kwenda kufunga sherehe ile, sheria iko wazi kuhusu utaratibu wa kupiga muziki maeneo ya baa na majumbani,” alisema Kamugisha.
Baadhi ya majirani waliozungumza na gazeti hili, walisema kumekuwa na tabia ya Diamond kufanya sherehe mara kwa mara nyumbani hapo, huku muziki mkubwa ukipigwa, jambo ambalo kwao ni kero.

“Nachukizwa sana na kelele za Diamond, kwani watu tunashindwa kulala kwa sababu yeye anafanya sherehe mbona kuna kumbi na hoteli anaweza kwenda tu, mimi nyumba yangu ni kama kilomita mbili kutoka kwake, lakini nasikia muziki kwa kero, je walio ubavuni mwake si wanataabika sana!” alisema mzee mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Gazeti hili lilimtafuta Diamond kwa simu yake mkononi ili kuzungumzia ishu hiyo lakini iliita bila kupokelewa kwa muda wote.

Source:Global
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. INAKERA NA SIO USTAARABU,NA TENA KWA MSANII MKUBWA KAMA DAIMOND ANGEWEZA KUTENGENEZA NYUMBA YAKE NDANI UKUMBI WA BILA KUTOA KELELE KWA JIRANI.

    ReplyDelete
  2. Ni kweli angeweza kutengeneza ukumbi wa ndani usiotoa sauti kuepuka kuwapigia kelele majirani zake,unapojenga nyumba lazima ujue na matumizi yake...

    ReplyDelete
  3. kweli kabisa Diamodnd jenga ukumbi wanaoita soundprouf sijui kama nimepatia jamani hilo neno maana lugha za watu bwana

    ReplyDelete
  4. chuki binafsi tu hizo hakuna lolote najua waswahili ndo zenu.....Dangote tafuta nyumba hamia masaki tu hao akina kajamba nani hawaataacha kukuletea vitimbi wanataka uishi kama wao pumbavuu zao. Eti kumbi za hotel zipo.....nani hua anaenda kukodi ukumbi hotelini kufanya birthday huko mivumoni shwaini zenu...........wabongo kasumba tu zimewajaaa na matakufa maskini

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe mwenzetu wa Taifa gani, naona umewatolea povu wabongo kama wewe huhusiki vile. Acha utumwa wewe

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad