Alichokiongea Waziri Nchemba Baada yakufika Eneo Walipouwawa Askari Polisi Dar

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Tukio la kuwawa kwa Askari Polisi wanne katika shambulio lililofanywa na watu wanaotuhumiwa kuwa ni majambazi usiku wa August 23 2016 zimeendelea kuchukua headline ambapo safari hii Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba alifika eneo la tukio ambapo pia Ayo TV ilipata nafasi ya kufanya naye mahojiano.

Waziri Nchemba amesema…
’Kumetokea shambulio la uvamizi lenye nia ya uovu ambalo limeua askari wanne, vijana wamefika na wataendelea na msako kuhakikisha waharifu wote wametiwa nguvuni‘
‘Tukio lilitokea majira ya saa moja na nusu usiku ambapo bado uchunguzi unaendelea na taarifa kamili itatolewa na Jeshi la Polisi, kifupi ni kwamba shambulio lilifanywa kwa kutumia usafiri wa pikipiki na niwakati vijana wakibadilishana lindo lakini niwahakikishie wananchi kuwa watuhumiwa wote watatiwa hatiani‘ –Waziri Mwigulu Nchemba
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Waziri nguo zake zimefanana na za polisi
    Kwani ni polisi?
    Tukiweka sheria basi iwe kwa wote

    ReplyDelete
  2. Polisi wetu ni wa kuzuia maandamano tuu na kuonea raia wasio na hatia

    ReplyDelete

  3. polisi waonyeshe ukakamavu kuzuia matukio kama haya..wameingia kwenye siasa wanaume wamepata mwanya wa kufanya yao sasa..

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad