Maafa Tena Kagera: Ugali wa Sumu Waua Mama na Watoto Wanne

MAMA na watoto wake wanne wamefariki dunia katika Kijiji cha Kyebitembe wilayani Muleba mkoani Kagera, baada ya kula ugali unaosadikiwa kuwa na sumu.
Waliofariki dunia ni Julitha Julius (35), Haujeni (14), Superius (12), Julius (4) na Paschazia mwenye umri wa miezi sita.

Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyamilanda, Trasias Baltromeo, alidai kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa tisa mchana.
Baltromeo alidai familia hiyo baada ya kumaliza kula walianza kutapika na walifariki dunia wakati wakipelekwa katika Kituo cha Afya cha Kimaya kilichoko jirani na kijiji hicho.

Alisema baada ya kula walianza kutapika na kuhangaika, hata hivyo wananchi walifika ili kutoa msaada wa kuokoa maisha yao lakini haukuzaa matunda ambapo walifariki.

ìNilipofika nilikuta hali si nzuri, nilikuta wakiwa wanatapika, hivyo nilitoa taarifa Kituo cha Polisi Kyebitembe ambapo walifika wakati wakiwa wanakimbizwa hospitali ndogo ya Kimeya ambapo mama yao na watoto wawili walifariki,îalisema.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera, Augustino Ollomi, alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na hakuna mtu aliyeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo.
Ollomi alisema miili ya marehemu inafanyiwa uchunguzi na wataalamu wa afya ili kujiridhisha na kutambua aina ya sumu iliyowaua.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Richard Ruyango, alisema jopo la wataalamu wa afya na Jeshi la Polisi walikwenda katika Kituo cha Afya cha Kaigara na Hospitali ya Rubya kufanya uchunguzi.

Alisema baada ya kufanya uchunguzi watalaamu hao hawakuweza kubaini aina ya sumu iliyokuwepo katika chakula hicho, hivyo wamechukua sampuli kwa ajili ya kupelekwa Ofisi ya Mkemia Mkuu mkoani Dar es Salaam, kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Mkuu huyo alikemea vitendo vya mauaji vinavyofanyika katika tarafa ya Kimwani kwani hilo ni tukio la tatu kwa mujibu wa vyombo vya dola la familia kuwekewa sumu kwenye vyakula na watu kupoteza maisha.

ìKitendo hiki kinasikitisha cha kuondoa uhai wa mwezio na si mafundisho ya Mungu licha ya waliofanya hivyo kuwa miongoni mwa waumini wa kiroho kwani wangetumia sheria kushitakiana kama hakuna usalama,îalisema.

Ruyango alisema Jeshi la Polisi na kamati za ulinzi na usalama za kijiji na kata, zimepewa jukumu la kufanya uchunguzi na kubaini waliohusika ili wachukuliwe hatua za kisheria.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad