YAMETIMIA...Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Limetangaza Kupunguza Idadi ya Wafanyakazi Wake

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limetangaza kupunguza idadi ya wafanyakazi wake ikiwa ni njia ya shirika hilo kuweza kujiendesha kwa faida na kufikia malengo yake.

Mkurugenzi Mkuu wa shirikia hilo, Mhandisi Ladislaus Matindi alisema kuwa mchakato wa kupunguza asilimia 90 ya wafanyakazi wa shirika umekamilika na utaratibu wa kuanza kulisuka upya shirika utaanza hivi karibuni.

Mkurugenzi huyo alisema asilimia 10 ya wafanyakazi watakaobaki ndio waliokidhi vigezo vinne walivyovitoa ambavyo ni uaminifu, elimu, uzoefu na kujali wateja.

Kwa upande mwingine alisema kuwa wafanyakazi wengine wameenguliwa kwa sababu hawawezi kwendana na kasi inayotakiwa kwa sasa na shirika hilo.

Kwa sasa shirika hilo lina wafanyakazi 221 ambao wanaelezwa kuwa ni wengi kuliko mahitaji halisi. Katika mpango huu wa kupunguza wafanyakazi, wanatarajia kupunguza takribani wafanyakazi 200.

Kuna taarifa ambazo bado hazijathibitishwa na shirika hilo kuwa tayari limewasimamisha kazi takribani wafanyakazi wote katika kituo cha nchini Comoro na kile cha jijini Mwanza.
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hapo kuna wizi mtupu na na kwa kweli hiyo Tanzania yetu ni shamba la bibi, inakuwaje Shirika la Ndege tena Ndege moja ya kukodi linaweza kuwa na wafanyakazi 221 kwa kweli huo ni wizi mtupu. Hela ya kuwalipa mishahara ilikuwa inatoka wapi???? Usiniambie kwa Ndege moja ya Kukodi ilikuwa inauwezo wa kurudisha gharama za uendeshaji wa Shirika na kubaki na faida juuu. Kwa kweli huo ulikuwa wizi wizi wizi wa hali juu ambao haujapata kutokea na kwa kweli haingiii hata akilini. Mashirika mengi ya umma ambayo yako chini ya Serikali yanatakiwa kuchunguzwa kama ni kweli ajira zake ni sawa na uwezo wa shirika husika katika kujiendesha na kupata faida juu. Kwa kweli bado kazi ipo.

    ReplyDelete
  2. :-) :-) :-) that is what it is going on now

    ReplyDelete
  3. Hiyo ndiyo bongo wana ujuzi uzoefu toka nchi ipate uhuru wake 1961 tunajiibia wenyewe na kusahau kuwa tunajikomoa wenyewe na vizazi vitakavyokuja vitatulaumu sana kwa kuja kulipa madeni yasiyowahusu

    ReplyDelete
  4. Wanaume tuko kazini. wala msiwe na shaka na awamu yetu hii ya tano. Haya yote na mengine hatuyafumbii macho. HAPA KAZI TU

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad