MKUU wa Wilaya Mdogo Kuliko wote Tanzania na Sifa za Mwanaume Anayetamani Kuolewa naye

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Zainab Abdallah, Mkuu wa wilaya ya Pangani ndiye kiongozi wa nafasi hiyo mwenye umri mdogo kuliko wote Tanzania, kwa sasa Zainab ana miaka 23 tu na bado hajaolewa lakini pia anazo sifa anazohitaji kutoka kwa mwanaume anayetamani kuolewa nae.

AYO TV na millardayo.com imempata Zainab Abdallah kwenye Exclusive na ameeleza jinsi anavyokutana na maswali mengi kuhusu lini ataolewa, nani ataolewa naye na je atakuwa na sifa zipi ili waendane.

“Nahisi nahitaji kuolewa na hata baadhi ya viongozi wameniambia Zainab utafika mbali sana lakini una mtihani mmoja tu unahitaji kuolewa, hilo ndio swali kubwa naulizwa. Unajua mimi ni binti mdogo lakini nimepanda sana kwenye siasa.”

“Kuna wakati nafikiria kuolewa na mwanaume ambaye hayuko kabisa kwenye masuala ya siasa, kwasababu tutaweza kuiweka sawa familia wakati mimi napokuwa kwenye kazi yeye atakuwa na muda na watoto, wakati mimi niko na watoto yeye atakuwa kwenye siasa, mwanaume ambaye ni mfanyabiashara labda au meneja wa taasisi fulani tena akiwa hajulikani nitakuwa salama zaidi” – Zainab Abdallah (DC Pangani) VIDEO:
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mmmh kumbe zai unataka wanaume wenye pesa sio mapenzi

    ReplyDelete
  2. Ana miaka 24 huyu duuuuuh basi hatari mi nikajua ana miaka 38 hv...

    ReplyDelete
  3. Ana miaka 24 huyu duuuuuh basi hatari mi nikajua ana miaka 38 hv...

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad