Mwendo wa Kupinga Tuu!! CHADEMA Kwenda Mahakamani Kuzuia Uteuzi wa Wabunge Wapya Uliofanywa na Magufuli

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

BARAZA la Wanawake la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha), limesema linakusudia kwenda mahakamani kuomba tafsiri ya sheria kuhusu uhalali wa Rais John Magufuli kuteua wabunge wawili wanaume wiki hii.

Wabunge walioteuliwa Jumatatu ni Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo na msomi wa sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Palamagamba Kabudi.

Mwenyekiti wa Bawacha, Halima Mdee, aliwaeleza waandishi wa habari jijini hapa jana kuwa hatua hiyo ya Rais, inakiuka matakwa ya sheria inayoelekeza kutenga nafasi maalum kwa wanawake.

Mdee ambaye pia ni mwanasheria na Mbunge wa Kawe, alinukuu baadhi ya vifungu vya sheria akisema katika nafasi 10 za uteuzi alizopewa Rais kisheria, anatakiwa kutenga nafasi zisizopungua tano kwa wanawake, jambo alilodai limekiukwa na Rais. 

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wa Bawacha, mpaka sasa Rais ameshazidisha idadi ya wanaume inayozidi nusu ya nafasi yake aliyotengewa kisheria ambayo ni wabunge 10.

Mdee alisema watawasilisha dai hilo mahakamani kupitia hati ya dharura kuiomba itoe zuio la wabunge hao wapya kuapishwa.

Kwa upande wake, Mbunge wa Bunda Mjini ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Esther Bulaya, alisema suala hilo linawahusu wanawake wote wakiwamo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na kuwataka waungane kudai mahitaji hayo ya Katiba.

“Hadi sasa, Rais Magufuli ameteua wabunge wawili wanawake akiwamo Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako na Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson kati ya wabunge wanane aliokwisha kuwateua... wanawake wote tuungane katika kudai haki yetu ya Kikatiba, hivyo UWT na Chama cha Wabunge Wanawake, wajitokeze," alisema Bulaya.
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad