Ubuyu wa Moto Moto!! Huyu Ndiye Waziri wa Magufuli Anayechepuka na Flora Mvungi,Walikutana Dodoma,Flora Akiri Kila Kitu Bila Kukataa

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

HUKU kukiwa na taarifa kwamba ndoa yake na msanii wa Bongo Fleva, Hamis Ramadhan Baba ‘H-Baba’ imeparaganyika, mrembo wa Bongo Movies, Flora Mvungi amedaiwa kunasa kwenye penzi la mmoja wa mawaziri wa serikali ya awamu ya tano.

 
Chanzo kilicho karibu na msanii huyo kimepenyeza habari kuwa, mrembo huyo kwa sasa yupo chini ya himaya ya waziri huyo (jina kapuni kwa kuwa hatujampata) ambapo safari ya uhusiano wao ilianzia mjini Dodoma.

“Nakumbuka ilikuwa ni mwaka jana, Flora alienda Dodoma na wasanii wenzake sasa alipofika mjengoni, waziri aliuona

mzigo hivyo akaomba nafasi na Flora bila hiyana akakubali.

“Mwanzoni kidogo alichomoachomoa lakini waziri alimuahidi maisha mazuri, na kwa kuwa tayari walikuwa kwenye gogoro na mtu wake(H-Baba), ilikuwa ni kama kumsukuma mlevi tu. Mtoto wa kike akaingia mzimamzima, yani sasa hivi Flora, kafa kaoza kwa mheshimiwa,” kilisema chanzo hicho makini.

Jitihada za kumpata waziri huyo ziligonga mwamba kufuatia simu yake ya mkononi kutokuwa hewani. Atakapopatikana, tutaripoti kwa upande wake ili kujua anazungumziaje madai hayo.

Kwa upande wake Flora, alipotafutwa na mwanahabari wetu alikiri kukutana na waziri huyo Dodoma lakini akaomba asizungumzie suala hilo kwani litamweka kwenye nafasi mbaya katika jamii.

“Naomba sana mliache hilo suala, najua aliyevujisha lakini nawaombeni sana mliache kabisa. Litanichafua tafadhalini sana,” alisema Flora.
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa umbea nanyi mmeliweka pamoja na kuombwa mliache kama lilivyo

    ReplyDelete
  2. JAMANI SAFARI YA DODOMA.. MIE KILA NIKIISIKIA NAIPENDAAAAA.. DODOMA OYEEEEE. DODOMA NDIYO TEGEMEO NA MATUMAINI YA KWETU SISI WOTE WATANZANIA.. NA MVUNGI KWAMBA AMEWAHI. NA WEWE USICHELEWE DODOMA NI DODOMA... KALIBUNI SANA DODOMA!!!!!! UNAIJUA DODOMA.. WATU WAKE NI WASTAARABU.. MIOYO YAO IKO WAZI...NI WACHAPA KAZI... HAWAMBUGUZI MTU NA WANAWAPENDA WOTE. NI WAKWELI NA WANAMPENDA MUNGU. KUTOKA KWA MATONYA NA YALEDI MPAKA KWA ASUMANI NA MWAMEDI HATA JONI NA FLEDI WOTE NI WAMMOJA NA UPENDO NA UNDUGU NI ZAO. kalibuni sana wandugu kwetu. ukitaka maji utapewa ..ukitaka tende na Halwa- shukua).. ukitaka nyama na utumbo -karibu) DONA NA SEMBE NDIYO SHAKULA YETU. KARIBU KWA MAZENGO NA LUSINDE WADODO WA KUKAYA. WAWALAMSAJE .. BAHATI YAKO MVUNGI INAANZIA DODOMA...WALA USINITAFUTE MIMI MWENYE NAJIJUA. FLORA WASIKUTUTIE PLESHA HAWA. HII NEEMA YA DODOMA.

    ReplyDelete
  3. JAMANI SAFARI YA DODOMA.. MIE KILA NIKIISIKIA NAIPENDAAAAA.. DODOMA OYEEEEE. DODOMA NDIYO TEGEMEO NA MATUMAINI YA KWETU SISI WOTE WATANZANIA.. NA MVUNGI KWAMBA AMEWAHI. NA WEWE USICHELEWE DODOMA NI DODOMA... KALIBUNI SANA DODOMA!!!!!! UNAIJUA DODOMA.. WATU WAKE NI WASTAARABU.. MIOYO YAO IKO WAZI...NI WACHAPA KAZI... HAWAMBUGUZI MTU NA WANAWAPENDA WOTE. NI WAKWELI NA WANAMPENDA MUNGU. KUTOKA KWA MATONYA NA YALEDI MPAKA KWA ASUMANI NA MWAMEDI HATA JONI NA FLEDI WOTE NI WAMMOJA NA UPENDO NA UNDUGU NI ZAO. kalibuni sana wandugu kwetu. ukitaka maji utapewa ..ukitaka tende na Halwa- shukua).. ukitaka nyama na utumbo -karibu) DONA NA SEMBE NDIYO SHAKULA YETU. KARIBU KWA MAZENGO NA LUSINDE WADODO WA KUKAYA. WAWALAMSAJE .. BAHATI YAKO MVUNGI INAANZIA DODOMA...WALA USINITAFUTE MIMI MWENYE NAJIJUA. FLORA WASIKUTUTIE PLESHA HAWA. HII NEEMA YA DODOMA.

    ReplyDelete
  4. waiting for your call 0787280120

    ReplyDelete
  5. hahahaaaaaaaaaaaa yuuuuwiiiiiiiiiii yaya gweeeee langa wasesya waiko waze walye zindozwa ze Dodoma kwa mzehe malecela

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad