HAPO awali ushindani kwa mastaa
ulikuwa ni ufahari katika maisha kama vile kushindana kuvaa, pesa,
majumba ya thamani na magari. Hali imebadilika hivi sasa, mastaa
wanashindana watoto, kila mmoja anataka mwanaye awe juu kumzidi
mwingine.
Tukianza na mtoto wa Nasib Abdul
‘Diamond Platnumz’, Princess Tiffa amekuwa gumzo kila kukicha kwa mtoto
mdogo kuwa na jina kubwa kuwashinda watoto wengine kutokana na ustaa wa
wazazi wake.
Mtoto wa Hemed Suleiman (PHD)
Hali hiyo imekuwa pia kwa mastaa wengine
ambao nao wanawaandaa watoto wao kuwa mastaa. Mtoto wa staa wa filamu
Bongo, Hemed Suleiman, anaonekana kuwa gumzo kwa kusifiwa na mashabiki
wa Hemed (PHD) kuwa mtoto huyo ni mzuri kuwashinda watoto wengine kwa
muonekano.
Dina Marious na mwanaye.
Aidha Babu Tale ameonekana mara nyingi
katika mitandao ya kijamii akiweka alama za mitihani ya mwanaye
zikionesha ufaulu wa mtoto wake. Mtoto wa Aunt Ezekiel na Moze Iyobo
dansa wa Diamond naye ametajwa katika watoto gumzo mtandaoni ambao
wanafuatiliwa na mashabiki wengi zaidi kutokana na ustaa wa wazazi wake.
Watoto was Zamaradi Mketema.
Wapo watoto wengi kama vile Mariam mtoto
wa MC Pilipili, Juju mtoto wa Zamaradi Mketema, mtoto wa Munaa Love,
mtoto wa Esma Platnumz na mzazi mwenzake Petit Man Wakuache, Mtoto wa
Tudd Thomas, mtoto wa Kajala, mtoto wa Faiza Ally, mtoto wa DJ Choka,
mtoto wa Dina Marious na wengine wengi.
Paula Paul mtoto wa ‘Kajala’ akiwana rafiki yake.
wa Zamaradi kiboko. Nawapenda sana.
ReplyDelete