Unaikumbuka Ile Story ya Madee ya Kupora Simu,Sasa Sikia Alivyojitetea Juu ya Tukio Hilo..!!!

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

Msanii wa bongo fleva Madee amesema hajutii matusi yanayotukanwa kupitia  mitandao ya kijamii kuwa amepora simu kwa kuwa wanaomtukana hawaujui ukweli na wakiujua watatulia.

Akionge kupitia eNewz Madee amesema hajapora simu bali alikuwa anadai pesa ambayo aliitoa kwa
 ajili ya kufanyiwa kazi na badala yake haikufanyika jambo lililomfanya aende kwenye vyombo vya sheria kwa ajili ya kurudishiwa pesa yake, na ndipo hayo yakatokea.

"Baada ya kuona pesa yangu ipo tu imekaa hafanyi kazi yoyote, nikafuatailia sheria, nikaenda polisi, nikasaidiwa kupata haki yangu, nashukuru nimepata haki yangu, wala sijutii kinachoendelea, sasa mi naweza kupora simu rafiki yangu, mi natumia simu yangi iPhone 7 na hiyo simu nayoambiwa nimepora ni S4, halafu kama ni kupora nisingeenda na polisi" amefafanua Madee

 Pia Madee amesema pesa yake huwa haipotei hata kama ikiwa imechukuliwa na maiti. 

Hata hivyo Madee amesema uongo huwa hauishi muda mrefu hivyo hawalaumu  wale ambao wamemtukana kwa kuwa hawaujui ukweli na anaamini kuna siku watu wote wataujua ukweli.
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tumekuelewa Madee! Haki unayo kama unavyoeleza.. Na udaku msukikilize Pande zote mbili kabla ya Shilawadu hawaja pokea stori kama hizi..Madee in Laisi wa Manzese na ni mtafutaji ajira kwa vijana wa manzese na usafi unaouona yeye ni mshiriki kamilifu.. Tuhuma hizi za mitandao hazina kichwa wala miguu na ni za Hovyo!!

    ReplyDelete
  2. Tumekuelewa Madee! Haki unayo kama unavyoeleza.. Na udaku msukikilize Pande zote mbili kabla ya Shilawadu hawaja pokea stori kama hizi..Madee in Laisi wa Manzese na ni mtafutaji ajira kwa vijana wa manzese na usafi unaouona yeye ni mshiriki kamilifu.. Tuhuma hizi za mitandao hazina kichwa wala miguu na ni za Hovyo!!

    ReplyDelete
  3. Majibu haya yana changanya niya kisanii kitupu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad