Waziri wa Nyerere ‘Amchana’ Magufuli

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
ARCADO Ntagazwa, aliyekuwa Waziri katika Serikali ya Awamu ya Kwanza, Pili na Tatu amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli, haina nia njema na wananchi wake, anaandika Moses Mseti.

Amesema moja ya kati ya mambo yanayothibitisha kuwa Serikali ya awamu ya tano haina nia njema na wananchi wake, ni msimamo ilionao kuwa Taifa halina njaa.

Ntagazwa ambaye aliwahi kutuhumiwa kuwa si raia wa Tanzania licha ya kuwahi kutumikia wadhifa wa uwaziri katika serikali ya awamu ya kwanza mpaka ya tatu kabla ya kushinda kesi, ametoa kauli hiyo leo alipozungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu.

“Kitendo cha Rais Magufuli kuwauliza wananchi wenya njaa kama wanataka akawapikie, kinasikitisha sana.

“Rais  hawapikii wananchi chakula jikoni, bali anaangalia utaratibu wa kuwatafutia chakula cha msaada katika wakati wa njaa, lakini yeye ameng’ang’ania na kila sehemu anasema hakuna njaa,” amesema Ntagazwa.

Mwanasiasa huyo mkongwe amesema kuwa ametembea katika mikoa ya Simiyu na Mwanza ambapo kuna ukame, hakuna mvua na mazao ya chakula yamekauka sana.

“Wananchi ndiyo ‘mabosi’ na ili uwe kiongozi bora ni lazima uwasikilize watu, lazima ufike sehemu yote ya nchi na uangalie watu wanavyoishi kuliko kuzungumza tu,” amesema.

Kuhusu utumbuaji wa majipu unaoendelea, Ntagazwa amesema mara nyingi Rais Magufuli amekuwa akifanya maamuzi ya kufukuza watu kazi bila kufuata utawala bora, utaratibu na sheria za nchi.

“Utumbuaji majipu si ajabu lakini lazima watumishi waongozwe kwa kufuata utaratibu na sheria za nchi zilizopo, utumbuaji huu si mzuri kwani unasababisha watumishi wengi wa umma wafanye kazi kwa woga badala ya kufuata sheria na taratibu,” amesema Ntagazwa.
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. naogopa kusema nisiende jela ila huyu rais kwa mda mfupi tushamchoka kabisa amekuja kuharibu vitu vingi alivyoasisiwa na wenzie waliomtangulia, mfano kwenye ajira kuzuia hasab walimu ameziumiza familia nyingi za kimaskini ila mungu atasikia kilio chetu watu wa hali ya chini

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umemchoka wewe, kwa kuwa ile mianya na ule ufisadi uliokuwa ukifanyika na kuiacha nchi pwaaaaa kwa si tiiii, hauipati au hamuipati, tena hamtoipata ngooooo!!! Shuwain wakubwa nyie. Mizoea vya kuchinja vya kunyonga hamviwezi, Twende kazini Raisi wetu jembe, wamalize kabisa wawe chaliiiiiiiiii. Kama si mbwataaaa!!! Wataijua Tanzania Miaka hiiii si ile ya mchezo mchezo kama michiii minglingen ya Africa. Iliyojaaa ouzo nao, ndio maana si ajabu kuambiwa akili zetu ndogo. Lete akili kubwa baba magufuri. Achaa na hao wenye akili ndogo, wasikusumbue walizoea ufisadi tu, lakini sio kwako

      Delete
    2. Sema UMEMCHOKAA sio TUMEMCHOKA

      Delete
    3. Uliemchoka ni wewe na mafisadi wenzako pumbavu zako wewe. Mlizoea kujimilikisha mali za Watanzania walio wengi na sasa mnakomeshwa mnabakia hapo kuhanyahanya wajinga nyie. Hiyo Nchi ni lazima irudi kwenye mstari ulionyoooka.

      Delete
  2. Huyu Babu naye mpumbavu ametokea wapi. Huyo Babu ni mmoja wa mafisadi wakubwa wa wakati ule na sasa imekula kwake anabakia kuzungumza mambo ya kijingajinga.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad