Mbunge Awalilia Watoto Wanaofanyiwa Vitendo vya Unyanyasaji

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

Mbunge Awalilia Watoto Wanaofanyiwa Vitendo vya Unyanyasaji
Mbunge wa Viti Maalumu wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Anatropia Theonest(Chadema) amesema watoto 244 wamefanyiwa vitendo vya unyanyasaji katika halmashauri hiyo kwa kipindi cha robo tatu ya mwaka huu.

Akizungumza leo, Agosti 13 Mbunge huyo amesema takwimu zilitolewa na Idara ya Ustawi wa jamii kwenye baraza la Madiwani zimeonyesha kati yao 85 walibakwa, 74 wakitelekezwa na 20 walilawitiwa.

Amesema matukio hayo yameongezeka kutoka 107 mwaka 2006 huku mtoto wa kike akiwa kwenye hatari ya kukosa haki ya elimu kutokana na kupata mimba.

"Ni lazima tusimame kwa pamoja tuweze kupaza sauti kwasababu tukiacha vitendo hivi viendelee tutajenga kizazi cha aina gani? cha walemavu?,"alisema

Aidha, amesema atawasilisha bungeni hoja binafsi ya kutaka marekebisho ya Sheria ya mwaka 1979 ili kuwapa haki watoto wanaopata mimba kupata haki ya kuendelea na masomo.


_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Eheeee... Anatropia!! Goodluck for your Mission. Lakini chonde chode Mama Glory usimwingilkie. Tumeshaona Unyatiaji wako. Wewe endelea na yako. Shauri yako. Mengine si Yako na Huko uendako Kazi Ni Yako. Kumbuka awamu hii ni Kazi Tu. DSalama yako ukifika uendayo kwa Miguu Yako. Mimba hatuzitaki Mashuleni ili tuepukane na Vilema kama Usemavyo. Ila Mama GLORY mlindie Heshima yake hata kama Umemtamani Mume Wake. Na ushike ADABU YAKO. ILI ULINDE MAADILI YAKO> Asante Anatropia Rwekila Theonest

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad