MECHI za Ligi Kuu Bara z i n a t a r a j i a kuendelea wikiendi hii kwa mzunguko wa nane kuchezwa, huku miamba miwili ya soka Tanzania, Simba na YanÂga ikitarajia kukutana kwenye Uwanja wa UhuÂru jijini Dar es Salaam, kesho Jumamosi.
Mchezo huu unataraÂjiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na timu hizo kuwa katika nafasi sawa ya msimamo wa ligi licha ya Simba kuongoza kwa idadi ya mabao ya kufunga, huku kila moja ikihitaji kukaa kileleni.
Mechi hii inatarajiwa kuwa ni ya vita na kisasi kutokana na hali jinsi ilivyo katika mechi husika ambapo kila upande utahitaji kuÂfanya vyema.
Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo yanatarajiwa kuifanya mechi hiyo kuwa ni ya vita na kisasi.
MAKOCHA KUTETEA VIBARUA VYAO
Imekaa vibaya kwa upande wa makocha wa timu zote mbili, kutokana na historia za timu hizo ambapo mara nyingi makocha wamekuwa wakifungashiwa viÂrago vyao pale wanapofungwa na wapinzani wao.
Hivi karibuni kulizuka uzushi juu ya Yanga kutaka kumuondoa koÂcha wake, George Lwandamina kutokana na matokeo mabaya katika mechi za awali jambo amÂbalo uongozi wa klabu hiyo ulikaÂnusha, lakini waswahili husema lisemwalo lipo, hivyo mechi hiyo inaweza kuwa katika wakati mguÂmu kwa upande wake.
Vilevile kwa upande wa Simba, Kocha Joseph Omog amekalia kuti kavu kwa muda mrefu kutoÂkana na uongozi wa klabu hiyo kutaka kumuondoa kutokana na madai ya kutokifundisha vyema kikosi hicho kwa kuona kuwa kimemzidi uwezo, lakini mkataba aliosaini umeonekana kumbeba kutokana na baadhi ya vipengele kuwabana waajili wake.
Hivyo basi, mechi hii ndiyo itakayotoa maamuzi juu ya kuenÂdelea kuwepo katika kikosi hicho kwa kuwa inadaiwa kuna kipengeÂle alichosaini kinaeleza kuwa iwapo t i m u haitaongoza msimamo wa ligi, itawapa nguvu viongozi kuweza kuvunja kandarÂasi hiyo.
Mshambuliaji wa Simba, Haruna Niyonzima akiopambana na wachezaji wa Simba.
Hivyo, atakuwa na kibarua kigumu kuhakikisha anafanikiwa kushinda mchezo huo ambao utakuwa na upinzani mkubwa.
KILA TIMU ITAHITAJI KUKAA KILELENI
Simba na Yanga zimefungana katika msimamo wa ligi kutoÂkana na zote kuwa na pointi 15, huku Simba ikiongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya mabao ya kufunga. Simba ina mabao 19 na Yanga ina mabao 10.
Hivyo, kutokana na jinsi msiÂmamo ulivyo, timu ambayo itashinda katika mchezo huo ndiyo itakayopata nafasi ya kuongoza msimamo wa ligi na iwapo itatokea wakatoa sare na Mtibwa Sugar yenye pointi 15 ikishinda mechi yao ya JuÂmapili dhidi ya Singida United basi itakaa kileleni.
KUONYESHANA UBORA WA VIKOSI
Kila timu inajinadi kuwa na kikosi bora ambacho imekisaÂjili msimu huu, hivyo mashabiki wanasubiri kwa hamu kubwa kuona timu gani itaonyesha ufundi zaidi katika mchezo huo.
AJIBU, NIYONZIMA & OKWI VIVUTIO
Kwa sasa habari ya mjini kaÂtika timu hizo ni kuhusiana na viwango vya wachezaji Ibrahim Ajibu wa Yanga na Haruna NiyÂonzima na Emmanuel Okwi wa Simba, hivyo kila mmoja atahiÂtaji kuona wanafanya nini kaÂtika mechi hiyo ya kesho.
Kwa upande wa Okwi, ndiye mchezaji kinara wa mabao kwenye ligi akiwa na mabao nane ambayo yameifanya kikoÂsi hicho kukaa kileleni kwa toÂfauti ya mabao.
Aidha, wachezaji Ajibu na Niyonzima, kwa sasa ni gumzo kutokana na viwango wanaÂvyoonyesha. Mashabiki wa timu hizo wamekuwa wakiÂrushiana maneno huku wale wa Yanga wakidai Simba wamepoteza mchezaji (Ajibu) kwani amekuwa muhimu JangÂwani na Niyonzima akipondwa kwa kuonyesha uwezo wa kaÂwaida tofauti na ule aliokuwa akionyesha Yanga.
HOFU YA MASHABIKI
Hofu kubwa ya mashabiki kuelekea mchezo huo, itakuwa namna ya kuingia uwanjani kwani kwa muonekano wa haraka Uwanja wa Uhuru jinsi ulivyo hauwezi kukidhi mahitaji ya mashabiki kutokana na udoÂgo wa uwanja huo tofauti na ule wa Taifa ambao ni mkubwa.
Kuna uwezekano mkubwa kwa mashabiki wengi kuangaÂlia mpira huo kupitia runinga kutokana na kushindwa kuÂingia uwanjani licha ya kuhitaji kuwaona wachezaji ‘live’ uwanÂjani.
Makala – Bongo: Khadija Mngwai, Dar Es Salaam