Wema Sepetu aendelea kuwa kimya baada ya Lipstick zake kufungiwa na Serikali

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Ni miaka mitatu imepita tokea Wema Sepetu Miss Tanzania 2006 azindue lipstick zake ziitwazo “Kiss By Wema Sepetu” na zikaingia sokoni na kufanya vizuri kwenye mauzo sehemu mbalimbali za Tanzania.

Leo November 11 2017 Serikali kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imetangaza kuzifungua lipstick hizo na kueleza kwamba wamebaini kuwa hazijakidhi viwango vya matumizi kwa binadamu.



Tulizoea kuona Wema Sepetu akijibu haraka au kuzungumzia matukio yake pindi tu yakitokea kama hivi lakini kwenye hili la leo bado ameendelea kuwa kimya na kutoandika chochote kulihusu kwenye mitandao yake.

Kwenye mitandao yake leo Wema ameichunia habari ya kufungiwa na badala yake ameendelea kuipigia debe APP yake mpya ya kulipia ambayo itakua ikionyesha mambo yake mbalimbali ikiwemo movie anazoigiza pamoja na maisha yake ambapo kwenye moja ya post zake alizopost jioni ya November 11 2017 imesomeka hivi hapa chini.

“Najivunia Kuwa The First Female in AFRICA to own my Very Own Application, Mnadhani naskia sifa wala… Sioni hata sifa… (LoveDove🤗🤗🤗 Download WemaApp now on Playstore… Soon itafika mpaka App Store… Inshallah“
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. jealous na chuki walizonazo kwa Wema lakini wasisahau kitu kimoja kimya cha mtu kina mshindo iaitoshe Mungu anaona kumfanyia mwenzenu ubaya kiasi hicho lakini wema atabaki kuwa wema na nyinyi endeleeni na majungu yenu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad