Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Japo hajataja jina, Wolper ameeleza kuwa mpenzi wake huyo ameridhia suala hilo kwani naye pia alikuwa akilihitaji toka mwanzo huku akibainisha kuwa amejifunza kunyamaza bila kuweka hadharani mahusiano yake na siku ya leo ndipo anatarajia kumtambulisha nyumbani kwao, Moshi na taratibu nyingine kama mahari kufuata.
ALICHOKIANDIKA WOLPER
“Wewe ni mwanaume ambae umejitoa ili tu niwe wako, umetaka tufike mbali kwanza kabla ya mambo mengine (uwende kwa wazazi, (NDOA) pamoja na kwamba mahusiano yangu ya nyuma yalikuwa yana misukosuko mingi ila umemthamini Jacq. Nilipotoka niliteswa sana na mapenzi yaani usaliti, dharau, kukosa na mapenz ya dhati.
“Pamoja ya kuwa pia alishatokea mmakonde na kunipeleka mapaka Mtwara na matembele nikachuma na wanakijiji kunipokea na kupikia familia na kutambulishwa kwa wazazi lakini sikufanikiwa kufikia hatua hii ambayo umefika, umenijali na umenisikiliza nilipokwambia sihitaji mtu bali nahitaji future husband,” ameandika Wolper.
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA