Joshua Nassari Avamiwa Nyumbani Kwake Usiku na Watu Wasiojulikana Waliokuwa na Silaha za Moto

Joshua Nassari Avamiwa Nyumbani Kwake Usiku na Watu Wasiojulikana Waliokuwa na Silaha za Moto
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari amedai usiku wa kuamkia Jumamosi hii alivamiwa na watu wasiojulika wakiwa na bundiki na kufyetua risasi nje ya nyumba yake.

Nassari amedai muda mchache baada ya tukio hilo yeye pamoja na mke wake walifanikiwa kufika kituo cha polisi na kutoa ripoti na tukio hilo.

“Nimevamiwa nyumbani kwangu maeneo ya USA RIVER usiku huu na watu wenye silaha, na kufyatua risasi ambazo zimeua mbwa waliokuwepo nje ya nyumba. Nimefanikiwa kukimbia na mke wangu na kuripoti kituo cha Polisi. Nimekuwa nikitishiwa kuuawa kila siku, sina amani ndani ya nchi yangu,” alitweet Nassari.

Amedai watu hao baada ya kufyetua risasi walifanikiwa kumuuwa mbwa wake ambaye alikuwa nje ya nyumba.

Mbunge huyo mara kadhaa amekuwa akiripoti katika mitandao ya kijamii kwa amekuwa atishiwa kuuawa mara kwa mara.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Pole Nassari, Wizi wameshapiga Dira kuwa wewe unaweka posho nyumbani.
    Hivyo benki huna Akaunti.
    Na Posho yako ni kiasi gani?
    na biasharea ya Filashi ina faida kubwa ndiyo maana wanarandia. Manake umeitangaza sana.
    Majambazi wako wengi mijini lakini kama ulivyo fanya ni sawa umetoa Ripoti na Wana usalama watalishughulikia.
    Nimekushauri usiitangaze Biashara yako mitandaoni manake hujui nani ni Mnunuzi na nani ni Feki.
    Na Kulewa kwako kwa kupita Kiasi Uwache.....!!! Manke unaweza kulala FOFOOOO na Ukaibiwa na ukitaka kujihami wakati wa Mwisho ndiyo Vile....

    ReplyDelete
  2. Mimi sio mtaalamu wa makosa ya jinai lakini hili tukio la kuvamiwa kwa huyu Nassari hakika lina kila dalili yakuwa ni mchezo wa kuigiza au movie alieitengeneza yeye mwenyewe na muhusika mkuu au staring ni yeye mwenyewe. Nassari watu watake kumua kwa tishio gani alinalo kisiasa? Labda majamabazi kutaka kumpora lakini niliangalia maelezo yake binafsi ya Nassari akilalama kana kwamba vyombo vya dola ndivyo vilivyo husika na tukio hilo. Jamani? Vyombo vya dola au serikali ikitaka kumfanyia uhalifu raia haiwezi kumkosa kwani wana watu ambao ni well trained sio rahisi mtu kama Nassari akajibizane risasi na usalama wa taifa au askari polisi alafu Nassari atoke salama hivyo ni vitu vya kuchekesha sana. Kuna sababu nyingi ya Chadema na Nassari kutengeneza hii movie inayoitwa watu wasijulikana. Sababu ya kwanza (1) siasa za matukio...baada ya Chadema na upinzani kukosa hoja za msingi za kushindana na CCM matukio yakuunda na ya kutengeneza ndio imekuwa mtaji wa kutafutia mvuto wa kisiasa kwa wanachama wao na wananchi. Sababu ya pili. Hakuna asiejua yakwamba chama cha Chadema kinakwenda zake kuzimu hilo halina shaka lakini wahusika wanataka kuaminsha ulimwengu yakwamba kufa kwa Chadema ni kutokana na uonevu wa serikali ya chama cha mapinduzi kitu ambacho sio kweli. Sera mbovu za Chadema. Muundo m'bovu wa chama ukanda na umimi ndio halibadri inayoiua Chadema. Sababu ya tatu ni..Siasa za hofu. Hofu ni mmoja ya kati ya mtaji wa maana katika harakati za kumiliki hisia za watu. Wakati mwengine hofu hutumika hata kutawala watu iwe katika mapenzi, ndoa, kazini nakadhalika hofu ni silaha muhimu . Chadema na upizani wanatumia hofu kama mtaji wa kisiasa ili kuvuruga mawazo ya watanzania ili waondowe imani juu ya serikali yao inayowaongoza. Sababu ya nne ya Chadema na upinzani kutengeneza siasa za matukio ni kujaribu kuzishawishi jumuiya za kimataifa baada ya kugonga ukuta hapo mwanzo yakwamba utawala uliokuwepo hivi sasa Tanzania si utawala wa sheria na haki ni wa udikteta, ni njia moja ya Chadema kujitafutia sapota na misaada kutoka mataifa ya nje hata kama ni kuichafua nchi yetu katika jumuiya za kimataifa. Ikumbukwe wazungu Mjerumani,Muengereza na wengineo walizitawala nchi za kiafrica na kuiba kila kitu mpaka watu kwa mamia ya miaka sio miaka mitano 5 au kumi 10 na hakuna waliposhitakiwa some time you can see how stupid as Africans we are in believing white people. Na kwa hili tukio la Nassari kila mtu anajua yakwamba kama uchaguzi utafanyika leo wa ubunge pale katika jimbo lake basi Nassari hawezi kushinda tena hata CCM wakimsimamisha mgombea mpumbavu . Hata matokeo ya chaguzi za madiwani, upinzani hawakuibiwa wala nini wamepigwa haswa kihalali kabisa na hata kama ukirejewa tena hii leo si ajabu Wapizani wakapoteza hata hicho kiti kimoja wichopata. Watanzania wamechoshwa kudanganywa na wapinzani. Wamechoshwa na ahadi hewa za wapinzani na wamebaini ili mabo yao yaende lazima wailete serikali karibu na wanapoishi. Na hawawezi kuileta serikali karibu na wanapoishi kama hayaja wachagua wagombea wa chama tawala. Na kwa bahati nzuri Magufuli anajitahidi kuhakikisha watendaji wake wanakuwa watendaji wa watu hasa wanyonge na kuhakikisha wanawajali. Katika falsa ya utendaji uliotukuka katika kuwahudumia wananchi,watendaji wa serikali siku zote huwa watumwa na wananchi ndio mabosi na serikali ya Magufuli inakaribia utukufu huo kwa hivyo upinzani bado unasafari ndefu kuin'goa CCM na katika kuchanganyikiwa huko kwa upinzani ndiko kunakowapelekea kuzua mambo wengi ya ajabu ili kusavaivu kisiasa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad