Maimatha 'Nitaendelea Kumfunda Hamisa Mobetto'

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
MTANGAZAJI maarufu Bongo, Maimartha Jesse ameibuka na kusema ataendelea kumfunda mwanamitindo Hamisa Mobeto ingawa amemjibu vibaya, kwani alichoamua ni kumshauri kwani anaona anakoelekea siko.

Akiongea na Risasi Jumamosi, Maimartha alisema kuwa alimshauri Hamisa kuwa makini kwani kuwa mgeni rasmi kwenye tamasha la Gal Power lililofanyika Uganda hivi karibuni halikuwa na hadhi yake na ilionekana yupo kwenye kushindana na Zarinah Hassan ambaye hamuwezi.

                           
“Kiukweli niliamua kumshauri na nitaendelea kumshauri ingawa alinijibu vibaya, lakini naamini ujumbe umemfikia na anatakiwa ajirekebishe na lile tamasha halikuwa na hadhi yake,” alisema Maimartha.

Hata hivyo, Maimartha alisema ataendelea kuwapa Kitchen Party mastaa mbalimbali ambao wanaonekana kwenda kinyume na wanavyotakiwa kuwa na anaomba watu mbalimbali wanaokerwa na tabia zao wapige kelele za kupinga ili zisiendelee.
Na Gladness, Mallya
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kweli ulimshauri na ushauri ulikuwa ni sasa kabisa but mbn kina bi sanura na genge lake huwashsuri ushindani lazima utakuwepo sio kwenye uke mualuko tu sio hadhi yake hata hao washindani sio hadhi yake hamisa ni binti kaleleka na ni mungawana kawavumilia sana navhuyu bi sanura ndie wakufundwa aki nyariwa kwa bi tukinau anahamisha jeshi kwa hamisa, jamani mnyonge mnyongeni na haki yake mpeni huyu nasebu si mume wa mtu na sio mtoto mdogo alipoamua kulala na hamisa hajajua matokeao yake? semeni kweli dunia ni duara bi sanura kaa uzingatie na huo mdomo wa kuropoka uvyo kitu kimmoja tu kumbuka ulipotoka jibu la mjinga ni ku kaa kimya waache wa rap wa snap mwisho watachoka kitu kinashangaza mtu mzima huzima sio mito unawaka na yeye anapalilia una binti yako na malipo ni duniani hao waganga wenu hawawezi kuwafaa moto unawangojea

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad