Maxence Melo: Utambulisho wa Majina Mitandaoni Utaua Habari za Kiuchunguzi

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Wadau wa majukwaa ya habari za mitandaoni, nchini Tanzania wameitaka Serikali kutafakari juu ya kasoro zilizoko katika Kanuni za Maudhui ya kimtandao.

Wakati wa mdahalo huo uliofanyika Jumamosi, Dar es Salaam, wadau hao walijadili mchango wa mitandao ya kijamii katika kuhamasisha utawala bora.

Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo alisema kipengele kinachotaka utambulisho wa majina ya washiriki katika mitandao ya kijamii kinalenga kuuwa upatikanaji wa taarifa nyingi za kiuchunguzi.

“Athari zake ni kwamba, utapata watu wachache watakaotoa taarifa za ufisadi ndani ya Serikali, hatuoni sababu za kutambua majina ya washiriki katika mitandao, itakuwa ni mwisho wa watu wengi kusema ukweli,” alisema Melo aliyesimulia harakati za kuanzisha jukwaa hilo takribani miaka 15 iliyopita.

Washiriki wengine katika mdahalo huo ulioandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), ni makundi ya vijana mbalimbali ya wafuasi wa vyama vya siasa, wanahabari na wanasheria. Pia walikuwepo watoa huduma na wamiliki wa majukwaa ya habari za mitandaoni, wasomi na watumiaji wa mitandao.

Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Rachel Yusuph alisema kanuni zenye adhabu kali siyo suluhusho la kurejesha nidhamu na uhuru wenye mipaka katika matumizi ya mitandao nchini.

Alisema elimu bado inahitajika kwa watumiaji wake ili kuwaondoa katika utamaduni wa matumizi mabaya ya mitandao hiyo.
_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Tags

Top Post Ad

Below Post Ad