Baba Amuua Mwanaye Kisa Parachichi

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa
Baba Amuua Mwanaye Kisa Parachichi
Polisi nchini Kenya linamsaka Mr. Morris Kirema kwa kosa la kumuua Mtoto wake mwenye miaka 12 na kumjeruhi Mtoto wake mwingine mwenye miaka 8 kwa kutumia panga na mateke akiwashutumu Watoto hao kula maparachichi kutoka katika shamba la jirani yao.

Mr. Morris anadaiwa kutumia mateke, ngumi pamoja na panga kuwaadhibu Watoto hao baada ya kula maparachichi kutoka katika shamba la jirani yao na kupelekea Mtoto wake huyo wa kiume mwenye miaka 12 kufa hapohapo.

Kwa upande wa Mtoto wa kike mwenye miaka 8 yeye amejeruhiwa vibaya sana pamoja na Mama yake ambao wanapatiwa matibabu katika hospitali moja nchini humo.



Inadaiwa kuwa mwenye shamba ambalo Watoto hao waliiba maparachichi hayo alidai alipwe kutokana na kitendo walichokifanya Watoto hao na ndipo Mr. Morris alipokasirika na kunuia kuwa lazima atawaua Watoto hao wakirudi kutoka shule.

Aidha duru za kuaminika zinasema kuwa Mwanaume huyo anasumbuliwa na uraibu wa michezo ya bahati nasibu na amekuwa akiwa mchungu akiombwa pesa na Mke wake
_________

LOVE STORY YA UTANIKUMBUKA NEYLA Ipo tayari ni maandishi na Sauti !, Kuisoma yote Bonyeza HAPA Lipia tsh 1000 Tu mtandao wowote,au Tembelea www.makapedia.com

Tags

Top Post Ad