Kampuni ya OYA Wafunguka Wafanyakazi WAKE Kufanya Mauaji Kisa Mkopo

Kampuni ya OYA Wafunguka Wafanyakazi WAKE Kufanya Mauaji Kisa Mkopo


Kampuni ya OYA Microfinance imekanusha kuwatuma wafanyakazi wake kumpiga hadi kumsababishia kifo mkazi wa mlandizi Wilayani Kibaha Mkoani Pwani Juma Mfaume tukio ambalo lilitokea Oktoba 7, 2024.


Tukio hilo ambalo limezua hisia kubwa lilipelekea jeshi la polisi kutoa taarifa ya kukamatwa kwa watu wanne ambao ni wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo.


Katika taarifa yake kampuni hiyo imeeleza kusikitishwa kwake kuhusu tukio hilo huku ikieleza kuwa kampuni hiyo haijawahi kuidihinisha wala kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wake kutumia nguvu katika urejeshaji wa madeni.


Taarifa hiyo imefafanua kuwa kampuni hiyo inafanya kazi kwa kuzingatia sheria na maadili huku tukio hilo halionyeshi maadili wala taratibu za kazi zao.


Katika taarifa yake, jeshi la Polisi limetoa wito kwa makampuni na taasisi za kifedha kufuata taratibu za kisheria katika kudai fedha kutoka kwa wateja wao ili kuepusha usumbufu na madhara yanayoweza kutoka ikiwemo uharibifu wa Mali, kujeruhi na vifo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad