Aliyemuua Osama aibuka

RISASI tatu zilimmaliza Osama bin Laden na kuandika historia.Karibu miaka miwili sasa, baada ya kimya na siri ya namna mauaji hayo yalivyofanyika, siri iliyofichwa imewekwa wazi kuhusu namna Osama alivyowapa kiwewe askari waliomvamia nyumbani kwake ambao walishindwa kumkamata akiwa hai tofauti na dhamira ya awali.

Askari aliyetekeleza mauaji hayo, tayari amefunguka na kueleza kwamba mshtuko alioupata alipokutana uso kwa uso na kiongozi huyo ulimsukuma kutekeleza mauaji yake.

“Nilimpiga risasi tatu. Nilimshuhudia akiwa amekufa ulimi nje. Nilimwona namna alivyokuwa akikata pumzi yake ya mwisho. Niliuliza akilini: Hivi hili ni jambo jema au ni jambo baya kabisa kuwahi kulifanya katika maisha yangu?”anaeleza askari huyo.

Askari huyo ambaye alipewa jina la the Shooter “mdunguaji” amesema hawakuwa na uhakika wa kumshinda, hadi walipofanikiwa kumtia nguvuni akiwa chumbani kwake katika uvamizi uliofanyika usiku wa manane.

Operesheni hiyo ilifanyika Mei 2, 2011 baada ya maandalizi yaliyowawezesha askari sita wa Marekani kumvamia kiongozi huyo wa kikundi la Al Qaeda aliyekuwa akisakwa kwa gharama zote na Marekani akiwa katika makazi yake huko Jalallabbad, Pakistan.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ungo osama kafa kwa ahad za allah sasa we endelea alshabab wajue unaongopa waulize kenya

    ReplyDelete
  2. hakuuliwa kamakufa alikufa kifo cha kawaida..kwajinsi marekani ilivyo wangepata hata maiti yake wangeizungusha dunia nzima kila mmoja ajue

    ReplyDelete
  3. Kwani asife ye si kiumbe hai? Acheni ubishi wa ajabu nyie watu......kwanini huwa amuamini mnavyoambiwa vitu au nyie ndo Mungu mnajua alivyokufa......kama kafa kwa kifo kingine kwanini haikutangazwa awali......acheni ubishi someni nyakati

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad