Hussein Machozi Amwita Diamiond Kuku Jike


‘Addicted hit maker’ Hussein Machozi amefunguka kuhusu uhusiano wake na Diamond platnumz na kuonesha kuwa hawana urafiki hata kidogo, japo hakusema moja kwa moja kama wana uadui na kwamba yeye na Diamond ni kama ‘Jogoo na kuku Jike’ na yeye Hussein ndiye jogoo!


Hussein Rashid a.k.a Hussein Machozi amefunguka kwenye XXL ya Clouds fm katika segment ya U Heard, alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu tuhuma zilizowafikia ‘Timu Makorokocho’ kuwa Hussein Machozi alipigana na Diamond Platinumz huko Mombasa.


Japo Hussein alikiri kuwa anauwezo wa kupigana kama bondia, lakini alikanusha kabisa kuwa hajawahi kupigana na Diamond na wala hajawahi kuzinguana nae, kwa sababu hawajawahi kabisa kuwa karibu, na sababu ni kwamba wanatokea katika sayari tofauti kabisa, yeye anatokea sayari nyingine na hajui Diamond anatokea sayari gani.


Japo aliongea kwa ufupi sana lakini hii ilitoa picha ya moja kwa moja kuwa inawezekana Hussein ana kitu moyoni ama hasira flani kuhusu Diamond Platinumz. Je wewe unamtazamo gani kuhusu hili?

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jaribu nawe kusaka habari uwe wa kwanza then nao wakuige kwani mara nyingi udaku wako tunaujua blog inahitaajika kupambana sana la sivyo utakosa wadhamini na kukosa mkwanja

    ReplyDelete
  2. Afunguke mwenyewe huyo husein kafanyiwa nini kwani?

    ReplyDelete
  3. Chozi jipe shughuli... Wivu kidonda wangu ukiushiriki utakonda...!!!

    ReplyDelete
  4. Habari sizizo na uhakika hatutaki

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad