"Mama yangu ndio mchawi wa Mafanikio yangu, Si Ndumba wala Wagaga" Diamond


Huenda ile story ya kwamba Diamond amepata na anaendelea kupata mafanikio kutokana na kutumia waganga wa kienyeji si kweli!! You never know! Staa huyu ambaye gazeti la Daily Nation limemtaja kuwa miongoni mwa wasanii wa Bongo Flava matajiri zaidi, yupo karibu mno na mama yake mzazi na pengine ndio maana anafanikiwa, nani kama Mama? Vipi kama mafanikio yake ni thawabu halisi kutoka kwa Mwenyezi Mungu?

Hizi ni picha ambazo Diamond ameziweka kwenye website yake na kuandika kwenye moja ya picha hizo: Siku zote kabla ya kwenda popote lazima tupitie kwa mama yetu mpendwa atupe Barka zake na nyingine hiyo juu akiandika: Nikipokea baraka za Mama ….Nijaliwe Mema….na Niende kwa Amani…!!

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hiyo picha Diamond amepiga kama geresha tu kutuonesha kuwa mama ndiyo kila kitu ktk mafanikio yake,mfano hiyo picha hapo juu ni baraka gani anazozitaka kutoka kwa mama wakati ana kapelo(kofia) kichwani?

    ReplyDelete
  2. si unajuwa hututaki kuona mmoja wetu kapata mafanikio ndo tunaaza kuchafuana kama ivii ila mimi nakukubali sana na hapa na skiliza track yako kamuwa waache waseme

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad