Msanii Jack Chuzi Adai Isabela Anatoka na Wanaume Walala Hoiiii
0
February 22, 2013
WAKATI kukiwa na bifu la chini kwa chini kati ya wasanii wawili Jack wa Chuz na Isabela, hali imekuwa tofauti ambapo Jack ameamua kufunguka na kudai kuwa msanii huyo ni malaya na analala na wanaume walala hao, huku akijifanya matawi ya juu.
Kauli hiyo imekuja mara baada ya mwandishi wa DarTalk, kuzungumza na Jack juu ya maneno ya chini chini yanayosambazwa na Isabela juu yake, yanayodai kuwa alisababisha kumuachananisha na bwana ake.
Jack alidai kuwa kamwe hawezi kutembea na wanaume wanatoka na msanii huyo kwani hawana ubora huku wengi ni walala hoi wasiyojiweza hata kimaisha.
Alienda mbali zaidi kwa kudai kuwa kutokana na hali ya uchafu aliyonayo msanii huyo, hakuna mwanaume analiyewahi kutoka na yeye anayeweza kumtamani kwani ana mwili ambao hata mvuto hauna.
“Sijawahi kutembea na bwana wa Isabela sasa inakuwaje anazungumza mambo ya uongo tena ya chini kwa chini hana lolote nahisi anatafuta jina yeye wanaume zake wote walala hoi sasa itakuwaje watoke na mimi wakati hawana cha kunipa,” alihoji Jack.
Hata hivyo kwa mujibu wa maneno ya Isabela alidai kuwa Jack aliwahi kumfanya asielewane na mpenzi wake baada ya kumtaka kimapenzi huku akijua wazi kuwa anatokana na yeye miaka yote.