Mwigizaji Johari Mjamzito? Dalili zawapa Shaka Marafiki zake


BAADA ya muda mrefu msanii wa filamu bongo Johari, akiwa anasaka mtoto, sasa inadaiwa kuwa tayari ni mjamzito na kati ya hiyo kuna siri nzito ya mwanaume anayetarajia kuzaa naye, kutokana na usiri mkubwa unaoendelea kutawala huku akificha watu wasijue kama ni mjamzito huku dalili zikijitokeza wazi.

Mwandishi wa DarTalk alipiga story na chanzo kimoja cha habari kilichopo karibu na msanii huyo, ambacho hata hivyo kilikataa jina lake lisitajwe, huku akisema kuwa msanii huyo ana dalili kubwa zinazoonesha ni mjamzito lakini hadi sasa hakuna anayejua ni wa nani.

Kilidai kuwa pamoja na yote msanii huyo hataki watu wajue kama ana ujauzito kwa madai kuwa anataka wajue pale utakapokuwa na miezi kadhaa au atakapoona kweli hali yake imebandilika.

Chanzo hicho kilisema kuwa hakuna mwanaume yeyote anayehisi ni mtu wake kwani msanii huyo amekuwa akifanya baadhi ya mambo yake kwa siri kubwa bila kuwashirikishwa hata rafiki zake kutokana na matukio ya kuibiana wanaume yanafanywa na wasanii bongo movie.

“Dah kuna dalili kubwa tunazoona kutokana kwa Johari na tuna imani kubwa kwamba tayari mjamzito sisi tunajua kwa sababu ni wanawake, lakini cha kushangaza hataki watu wajue kama ni mjamzito lakini kubwa zaidi hatujui ni ujauzito wa nani,” alidai mmoja wa rafiki zake.

Hata hivyo alipotafutwa muhusika wa ishu hii ambaye nai Johari, alishindwa kusema lolote kwa madai kuwa yuko bize ingwa aliweka wazi kuwa kuna hali ya kutojisikia vizuri ila hajui kama ni ujauzito kama rafiki zake wanavyodai.

“Dalili hizo nimeanza kuzipata hivi karibu na bado sijajua kama ni mimba lakini kama ikiwa kweli nitafurahi maana napenda sana kuwa na mtoto umri wangu unaruhusu hivyo,” alidai Johari.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ili limejichubua au..kinyaa

    ReplyDelete
  2. Hongera yake kama itakuwa ni mimba kweli

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad