Ridhiwani Kikwete Nae Amjibu John Mnyika"Nimekuelewa Mbunge Wangu Mnyika"

 NIMEKUELEWA MBUNGE WANGU MNYIKA
Nimeisoma vizuri taarifa ya bwana Mnyika na nimeielewa. Nimeona sababu za msingi kwa nini hakumaliza shule na majibu juu ya hoja ambayo aliisimamisha bwana Nape Nnauye.

Ni jambo zuri ambalo amelifanya maana tumefunguka na kujua ukweli. Lakini naomba radhi kama sikueleweka vizuri. Nilichofanya mie ni kumuita ukumbini ili atutoe wasiwasi hasa mimi kama nilivyojielewa kuwa nilikuwa naye chuoni na ninaheshimu sana uwezo wake wa ufahamu.

Mwisho nimuhakikishie, ni jukumu la CCM kuhakikisha kuwa maji yanapatikana Jimboni Ubungo na tutayaleta. Kubwa zaidi akumbuke ilani yetu ni ya miaka mitano na maji yatafika pale kabla ya 2015. La msingi aendelee kuisukuma serikali na kumkumbusha waziri maghembe juu ya utekelezaji wa ya maneno yake mazuri na sio mbwembwe za kufurahisha baraza.

Mwisho, nikupongeze mnyika kwa kuja hadharani na kutoa wingu. Ni imani bwana Nape na wasomaji wengine tumekuelewa.

Shukrani. Hatuchafuani, tunasaidia kuwekana sawa . Huu ndiyo uwazi kwa vitendo.hongera muhes

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ridhiwani wewe ni wakili lkn uelewa wako unanitia shaka sana mnyika ameeleza na amemaliza shule wewe unasema umeelewa ni kwa nn hakumaliza shule sasa nani mbumbu kati ya ridhiwani na mnyika mimi naona ridhiwani wewe bado shukuru mdingi kakubeba.

    ReplyDelete
  2. Na yule mdogowako aliepataga O yuko wapi?

    ReplyDelete
  3. Ah hivi na wewe upo kwenye utekelezaji wa ilani za hyo chama ya dingi?..aah okeey nlitaka kusahau kua mtoto wa fisa..ah samahani,mtoto wa jk nae ni jk..nimekuelewa Rais mdogo!

    ReplyDelete
  4. That is the protection of incompetent personnel. I wonder how an advocacy is done if u received a writen document but failed to make interpretation, may be u end up half a story and concluded cauz story was to long. And thus how we failed to reach conclusion and end up by signing the void contract

    ReplyDelete
  5. Mi nikiwa mkazi wa Segerea tunakusudia kufungua kesi dhidi ya DAWASCO. kwa kusababisha hasara kubwa ya Tshs billion 200 kwa kutandaza mabomba ya maji ambayo hayajawahi kutoa maji na kwahivi sasa yameanza kuharibiwa na mmonyoko wa mitaro

    ReplyDelete
  6. kuwa mtoto wa rais si kuwa na akili liwe wazi hilo

    ReplyDelete
  7. Hawajui nn wanasema ulewa wao mdogo M4C never die

    ReplyDelete
  8. Kama huyu mtoto wa nyoka yy kama nani kuhukumu wengine. Anapendeza sana akuwa na kina wema na warembo wengine hapendizi kwenye jukwaa la siasa,hana mvuto pia hana busara

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad