Video: Q-Chief Amjibu Diamond: ‘He is a Good Kid, I love His Music, Siamini Katika Uchawi’


Baada ya jana Diamond Platnumz kufunguka kwa undani jinsi anavyochukizwa na kitendo cha mwanamuziki mwenzie Abubakar Katwila aka Q-Chief kumsema anatembelea nyota yake, Q-Chief amezungumza na Bongo5 kujibu shutuma hizo.

Katika kipindi cha XXL cha Clouds FM jana, Diamond alisema, “mimi sipendezewi na navyowaambia watu kuwa mimi namroga, kwanini nisitembelee nyota ya watu kama akina Omary, akina Ben Pol. Alumbane na wakubwa wenzie akina Dully Sykes, mimi sitaki, namheshimu abishane na wakubwa wenzie, mimi mdogo aniache na wadogo wenzangu.”

Akijibu shutuma hizo, Q-Chief amesema:

“Sijui wakati anajibu hayo maswali alikuwa kwenye hali gani, sijui alikuwa amekasirika, sijui alikuwa out of mood sijui alikuwa okay, lakini all in all najua kila mtu ana uhuru wa kuongea kile anachojisikia na hajawekea mipaka, as long as kinamsatisfy yeye na kinawafurahisha wengine kwenye umma.


Video hii Hapa:

Mimi watu wangu wamenichukulia positive hili jambo baada ya kusikikiliza walinirekodia nikasikiliza lakini am not a big fan of superstition so siamini hivyo vitu lakini kitu ambacho naweza kusema huu najua ni mchezo mchafu na acha niucheze kwa hisia kwasababu sijui huko mbele ni kitu gani kitakuja kunisaidia katika maisha na kunyamaza pia wakubwa wanasema ni ustaarabu. He is a good kid, I love his music, he is doing good.”

Pia Q-Chief ambaye wiki iliyopita aliachia wimbo mpya uitwa Akuro amesema atafurahi kumuona Diamond anakuja kwenye show yake ya kwanza tangu miaka mitano iliyopita itakayofanyika kwenye ukumbi wa New Maisha Club, Jumapili ya February 24.

“Ningependa awepo kwenye hii show aangalie kwasababu mimi pia nimekuwa nikihudhuria na nimeshawahi kufanya show ya Diamonds are Forever naye aliniita kwa mapenzi yake and with open-hearted I did a good show,” amesema Q.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad